Jumanne, 14 Juni 2016

KATIBU WA UVCCM MKOA WA IRINGA AWATAKA VIJANA KUJIUNGA KATIKA VIKUNDI ILI KUNUFAIKA NA FURSA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI






Baada ya kuwasili kata ya Kibungu kwa ajili ya kikao akitokea kata ya Ihalimba


 Katibu na viongozi wa ccm kata ya wakielekea kwenye chumba cha mkutano




 Katibu  umoja wa vijana Abdukarimu pamoja kisaini katika kitabu cha wageni

 

 Mwenyekiti wa umoja wa vijana ccm wilaya ya Mufindi Felx Lwimbo akizungumza na viongozi wa vijana katika kikao



 Katibu wa umoja wa viajana ccm mkoa wa Iringa Abdukarim Alamga akizungumza na viongozi wa umoja wa vijana kata ya Ihalimba
 


Ofisi ya chama cha mapinduzi ccm kata ya Kibengu




 Katibu wa umoja wa Vijana ccm  [Uvccm ]Mkoa wa Iringa Abdukarimu Alamga amewataka vijana nchini kuhamasika kujiunga katika vikundi vilivyosajili na  kuunda vipya ili vipate ujasili na hatimae waweze kunufaika na fusla zinazotolewa na serikali ikiwa ni pamoja na mikopo ya fedha.
Akizungumza na viongozi wa umoja wa vijana wa ccm  kata ya Ihalimba na Kibengu zilizopo jimbo la Mufindi kusini Halmashauri ya wilaya ya Mufindi Mkoani hapa, ikiwa ni moja ya ziara yake aliyoifanya jana ikiwa ni mwendelzo wa ziara yake ndani ya mkoa wa Iringa.
Alamga alisema kuwa  lengo la ziara hiyo ndani ya mkoa wa Iringa ni kuhamasisha vijana waweze  kuamka na kufanya kazi kwa bidii na kuwahamasisha wale ambao hajawajiunga katika vikundi vya ujasiliamali wajiunge ili waweze kunufaika na mikopo imnayotolewa na serikali, kuachana na tabia ya kukaa vijiweni na kuilaumu serikali kila kukicha
‘’’’’’Bajeti ya fedha 2016\17 imeshasomwa bungeni na sote tumeisikia, ndani yake kuna utekelezaji wa ahadi ya Mh.Rais aliyoitoa wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu 2015 kwa kupitria irani ya chama cha mapinduzi ccm kuhusu Mil.50 kwa kila kijiji.Fedha hizo zinatarajia kuanza kutolewa mwezi julai 2016 na zitawanufaisha waliojiunga katika vikundi vya mbalimbali vilivyosajiliwa kihalali,hivyo ninawasihi vijana muamke na kuchangamkia hiyo fulsa’’’’’’’’ alisema
Alisema  ni jambo la kushangaza kijana kuwa tegemwezi wakati kila mwaka asilimia 10 za fedha zinatengwea kwa kila Halmashauri nchini ,ambapo  asilimia 5 ni kwaa ajili ya vijana na asilimia 5 ni kwa ajili ya akimna mama lakini inasikitisha kuona kuona vijana kila kukicha wanalalamika  ugumu wa maisha,aliwataka nawaomba  waamumke  na kujiunga  ili waweze kupata  mikopo kwa  ajili ya maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Aidha  Katibu  huyo aliongeza kuwa,chama cha mapinduzi ccm kinatarajia kufanya uchaguzi wake ndani ya chama 2017  kwa mujibu wa katiba inavyosema,aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali bila kuogopa  kwasababu kuchagua na kuchaguliwa ni haki ya kila mwanachama wa ccm
‘’’’’’’’ Tunapoelekea uchaguzi mkuu ndani ya chama tunatakiwa kluiwa makinini sana  kuwachagua viongozi bora watakaokitendea haki chama chetu kwa kufanya jkazi kufuata kanuni na taratibu zilizopo katika Irani  ili kisiyumbe,Vijana  mna nafasi kubwa  katika uongozi,hivyo jitokezeni kuwania nafasi  za uongozi ndani ya chama ili tuijenge ccm Imara’’’’’’alisema

Kazi kubwa ya umoja wa vijana ccm ni ulinzi wa viongozi ndani ya chama na kufanya kazi za chama,hivyo vijana tunatakiwa  kujiunga kwa wingi ili tuweze kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali mara tu uchaguzi utakapotangazwa 2017
Alisema Chama cha mapinduzi ccm  lazima kisimamie  na kuhamasisha utendaji  wa  serikali kuanzia ngazi ya chini kwasababu  utekelezaji wake unatokana na Irani ya chama cha Mapinduzi,hivyo viongozi wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na  Irani inavyosema  na si vinginevyo.
Felx Lwimbo ni mwenyekiti wa umoja wa vijana uvccm wilaya ya Mufindi aliwataka viongozi  wa chama  katika kata hizo kubadilika mara moja  kwa kufanya vikao vya mara kwa mara ili   kuleta uhai wa chama ndaini ya mitaa yao.
Kwa wale viongozi wenye tabia ya kufanya kazi kwa mazoea huu siyo wakati wake,hatuwezi kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya Tano chini ya uongozi wake DR.Magufuli kwa kufanya kazi kwa mazoea.Zalisheni wanachama wapya na kuwahamasisha wajiunge katika vikundi ili waweze kupata mikopo.
‘’’’’’Natoa  14 kwa viongozi wa serikali ndani ya kata na chama  muhakikishe vikundi vyote ambavyo havijasajiliwa viweze kusajiliwa  ili fedha zitakapokuja  kuanzia hizi zainazotolewa na kila wilaya na mill.50 za Mh. Rais za kila kijiji  wananchi waweze kupata kutokana na vikundi vyao’’’’’alisema








































































































































0 maoni:

Chapisha Maoni