MAHAKAMAya Hakimu Mkazi iringa imemhukumu Erick Philipo (35)mkazi
wa kata ya Mkazi wilaya ya Iringa mkoani hapa kifungo cha maisha baada ya
kukutwa na hatia ya makosa matatu
likiwamo la kumlawito mtoto wake wa kike wa kumzaa mwenye umri wa miaka saba.
Akisomo hukumu hiyo jana Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Andrew
Scout alisema mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa
mashitaka mabao haujaacha shaka kuwa mtuhumiwa alitenda makosa hayo matatu kwa
pamoja.
Makosa mengine katika kesi hiyo namba 72 ya mwaka 2015 ni pamoja
na kuzini na ndugu yake kinyume na kifungu cha 227 sehemu
ndogo ya ya tatu ya sheria ya ushahidi wa mtoto na kosa la tatu ni
kumsababishia maaumivu mtoto huyo kinyume kifungo hiocho hocho
sehemu ndogo ya saba ya sheria ya ushahidi wa mtoto.
Scout alisema kutokana na ushaidi
uliotolewa mahakamani hapo, mtuhumiwa ametiwa hatiani kwa makosa yote matatu na kwamba katika kosa la pili ambalo ni
la kulawiti anahukumiwa kifungo cha maisha jela.
Adhabu nyingine katika kesi hiyo ni kosa la kwanza la kufanya
tendo la ndoa na ndugu yake ambapo alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jera na la
tatu ni la kumsababishia maaumivu mlalamikaji ambapo alihukumiwa kifungo cha
miaka mitano na kwamba adhabu hizo zitatkwenda pamoja.
“Katika kesi hii upande wa mashitaka ulioleta mashahidi nane na
upande wa utetezi ulileta mashahidi 7,baad aya kusikiliza pande zote mbili
upande wa mashitaka na jamuhuri,upande wa utetezi haujatoa ushahidi unaoweza
kuishawishi mahakama kutomtia hatiani mtuhumiwa”alisema Scout.
Katika kesi hiyo upande wa jamuhuri uliongozwa na mwanasheria wa
serikali Hope Charlesi aliyekuwa akisaidiwa na Happenes Flavian ambapo.
Wakili Charles aliitaka mahakama kumpa adhabu mtuhumiwa huyo
kulingana na sheria zinavyotaka huku mtuhumiwa alipopewa nafasi ya kujitetea
aliitaka mahakama kumpunguzia adhabu kwa mdai kuwa yeye anafamilia ya watu sita
wanaomtegemea.
Katika hatua nyingine Mahakama hiyo ilimuhukumu kifungo cha miaka
30 jela Johnface Lyang’oka baada ya kukutwa na
hatia katika makosa mawili likiwamo la kukutwa na hatia ya kujihusisha na
biashara ya Meno ya Tembo kinyume na sheria ya wanyamapori namba tano ya mwaka
2009.
Katika kesi hiyo alidaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa na maneo 32
ya Tembo yenye thamani Sh 516 milioni na katika kosa la pili mtuhumiwa huyo
alikutwa na vipande viwili vya pembe za ndovu vyenye thamani ya Sh 32.25
milioni.
Mtuhumiwa huyo pia ambaye katika kesi
hiyo namba …alishitakiwa alishitakiwa pamoja na mtuhumuiwa namba moja Alfani Balo bani ambaye aliachiw ahuriwatuhumuwa
Kosa la pili mntuhumiwa huyo alikutwa na Vipande viwli vya pembe
za ndovu kinyume na sheria vyethamani ya Sh 32 milioni kinyume na sheria ya
uhujumu uchumi.
Katika shitaka hilo lililofunguliwa mahakani hapo Septemba 11
mwaka jana mtuhumiwa huyo alishitakiwa pamoja na
mtuhumiwa namba moja ambaye ni Alfani Balobani ambaye mahakama ilimuachia huru
baada ya kutomkuta na hatia.
Mara baada ya kutolewa kwa hukumu hizo mbili Mkuu wa Wilaya ya
Iringa Richard Kasesela ambaye alikuwa mahakamani hapo kusilikiza hukumu
ya kesi ya ubakaji alielezea kufurahishwa kwake na hukumu hizo na kudai ni mwanzo mzuri wa kampeni dhidi ya vitendo vya ubakaji
na unyangilki dhidi ya wanyama..
“Nimefurahishwa sana hukumu za leo
,mahakama imetenda haki ,kumekuwa na kesi nyinge za
vitendo vya ubakaji na kupitia kesi hii mapambano dhidi ya watuhumiwa wa
ubaakaji ndo yameanza”alisema Kasesela na kuongeza:
“Kuanzia sasa ninapiga marufuku mtu yoyote hususani wanandugu
kumaliza kesi inayohusiana na vitendo vya ubakaji nyumbani na
atakayebainiaka kufanya hivyo atachukulwiwa hatua kali za kisheria”alisema.







0 maoni:
Chapisha Maoni