Jumatano, 1 Juni 2016

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO VYA HABARI


msangi_New1SACP: AHMED MSANGI
…………………….
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATU [3] WANAOJIHUSIHA NA BIASHARA ZA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI NA WENGINE [7] WANAOTUHUMIWA KULETA FUJO.
KWAMBA MNAMO TAREHE 30.05.2016 MAJIRA YA SAA 14:00hrs KATIKA MAENEO YA MIHAMA – MNARANI KATA YA KITANGIRI WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA RAYMOND MONGESA MIAKA 18 MKAZI WA MNARANI AKIWA NA MISOKOTO 30 PAMOJA NA KILO 10 ZA BHANGI, NA MWENZAKE DIONIZI ELIAS MIAKA 27 MIHAMA AKIWA NA MSOKOTO 01 WA BHANGI KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA ZA NCHI.
AIDHA BAADA YA KUWAKAMATA WATUHUMIWA HAO ASKARI WALIENDELEA NA DORIA PAMOJA NA MISAKO YA KUWASAKA WAHALIFU AMBAPO NASIBU ABDUL NA WENZAKE 07 WALIKAMATWA WAKIFANYA FUJO NA KUBUGUDHI ABIRIA KATIKA  MAENEO YA MECCO STAND, PAMOJA NA  MATHIAS MSUKUMA MIAKA  30 MKAZI WA NYAKATO SOKONI ALIEKAMATWA NA MISOKOTO  20 YA BHANGI.
WATUHUMIWA WOTE WAPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI DHIDI YA UHALIFU WA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA BHANGI ILI KUWEZA KUKAMATA WAHUSIKA WENGINE ZAIDI WANAOSHIRIKIANANAO KATIKA BIASHARA HIYO, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU MASHITAKA YANAYOWAKABILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA HASWA VIJANA KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU ZA MADAWA YA KULEVYA KAMA BHANGI NA ZINGINE  KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA ZA NCHI, KWANI JESHI LA POLISI TUMEJIPANGA KUHAKIKISHA TUNAKAMATA WAHALIFU WA  AINA KAMA HIYO  KATIKA SEHEMU ZOTE ZA MKOA WA MWANZA, HIVYO TUNAOMBA WANANCHI WATUPE USHIRIKIANO WA KWA KUTUPA TAARIFA MAPEMA ZA UHALIFU NA WAHALIFU ILI TUWEZE KUWAKAMATA NA KUWAFIKISHA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
IMESAINIWA NA
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

0 maoni:

Chapisha Maoni