Mkuu wa Wilaya ya Ilala,
Raymond Mushi akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya mazingira
duniani ambapo manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Kampuni ya usafi ya
Green Waste Pro Ltd na nyingine kwa kufanya usafi katika fukwe za
bahari ya Salender jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa
Serikali ya Mtaa wa Sea-View Upanga, Victor Muneni na kulia ni Afisa
Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
wa Sea-View Upanga, Victor Muneni akizungumza jambo na wadau wa
mazingira waliokusanyika kwenye viwanja vya Salender Club kabla ya
kuanza zoezi la usafi wa mazingira.
Baadhi ya wadau wa mazingira
kutoka ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, makapuni ya usafi
yaliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala ikiwemo Green Waste Pro
Ltd, Vijana kutoka Roots and Shoot waliokusanyika kwenye uzinduzi wa
wiki ya mazingira duniani iliyozinduliwa jana duniani kote.
Kiongozi wa dhehebu la Dawoodi Bohra nchini, Bw. Zainuddin
Adamjee (wa pili kushoto) akimtambulisha Kiongozi Mkuu wa dhehebu la
Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin (wa
tatu kushoto) kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kulia) mara
baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine (kushoto) akitoa salamu za serikali kwa
Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Bohora duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal
bhaisaheb Saifuddin aliyewasili jana jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akielezea mipango ya
manispaa ya Ilala katika kuweka jiji safi wakati wa hafla fupi ya
kukabidhiwa ‘Dustbin’ 53 zilizotolewa na Burhani Foundation Tanzania
iliyofanyika katika mskiti wa dhehebu la Mabohra nchini.
Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Dawoodi Bohra duniani, Ali
Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin moja ya Dustbin kati ya 53
zilizotolewa na Burhan Foundation kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond
Mushi katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwa Kiongozi huyo jijini
Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akimshukuru Kiongozi
Mkuu wa dhehebu la Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal
bhaisaheb Saifuddin kwa zawadi ya kikoi.
Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw.
Abdon Mapunda akipokea zawadi ya kikoi kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa
dhehebu la Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb
Saifuddin.
0 maoni:
Chapisha Maoni