Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki
Ulisubisya akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili (MNH) LEO. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamedi
Janabi, Katibu wa baraza hilo, Dk Kissa Mwambene. Kushoto ni Mwenyekiti
wa baraza hilo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru na Mkurugenzi wa Rasilimali
Watu wa MNH, Makwaia Makani.PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI (MNH)
Wajumbe
wa Baraza la Wafanyakazi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakipiga
makofi wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo Jinsia, Watoto
na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya wakizungumza na wajumbe wa baraza hilo
Leo kwenye hospitali hiyo.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa
Lawrence Museru akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi LEO
kabla ya kupiga kura za kuwachagua viongozi wapya wa baraza hilo.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia Makani wa
hospitali hiyo.
Wajumbe
wa Baraza la Wafanyakazi la MNH wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru katika kikao hicho.
Kutoka
kushoto ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa hospitali hiyo, Dk Kissa
Mwambene, Mwenyekiti wa baraza hilo, Profesa Lawrence Museru, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki
Ulisubisya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI), Profesa Mohamedi Janabi, Katibu Msaidizi wa baraza hilo,
Wakili Eneza Msuya na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia
Makani.
………………………………………………………………………………………………….
Katibu Mkuu Wizara ya Afya ,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya
ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuboresha maslahi ya
watumishi wake na kuendelea kuweka miundombinu bora ya kiutendaji.
Akizindua Baraza la Wafanyakazi
la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dk. Ulisubisya amesema hatua
hiyo ni ya kupongezwa kwani inampa motisha mtumishi kufanya kazi kwa
bidii.
“Nimefarijika sana kuoana
suala la maslahi ya watumishi linapewa kipaumbele hapa MNH kwa kweli
mnastahili pongezi na taasisi nyingine hazina budi kuiga mfano huu,
lakini napenda kusisitiza kuwa kila mtumishi ni vema akanufaika na
maboresho haya amesema,” Dk Ulisubisya.
Akizungumza kabla ya uzinduzi
wa baraza hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili, Profesa Lawrence Museru amesema hivi sasa hospitali hiyo
imeongeza mapato yake kutoka Shilingi Bilioni 2 hadi kufikia Bilioni 4.
Pia amesema katika kuendelea
kuboresha huduma za matibabu MNH ina mpango wa kuongeza ICU ya watoto
wadogo pamoja na ICU ya kina mama wenye matatizo ya uzazi ili kuokoa
maisha ya mama na mtoto .
Kwa mujibu wa Profesa Museru
Hospitali hiyo ipo katika hatua za mwisho za kupata mkopo kutoka Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkopo ambao utasaidia kupanua huduma
za afya ikiwamo kununua vifaa tiba vya upasuaji.
Katika kikao, wajumbe wa Baraza
la Wafanyakazi wamemchagua Dk. Kissa Mwambene kuwa Katibu wa Baraza
hilo pamoja na Eneza Msuya kuwa Katibu Msaidizi.
0 maoni:
Chapisha Maoni