SHIRIKISHO la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Chadema (CHASO) Mkoa wa
Iringa kwa kushirikiana na baraza la vijana chadema Mkoa huo (BAVICHA)
wameitaka serikali kupitia Wizara ya elimu kuwarudisha haraka wanafunzi wa vyuo
kikuu ha Dodoma (UDOM) ambao walirudishwa nyumbani juzi ili waweze kuendelea
kupata haki yao ya msingi ya kuendelea kupata elimu ili wakawahudumie wananchi
kama ilivyokusudiwa.
Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu
wa baraza la vijana Chadema (BAVICHA) Mkoa wa Iringa Jackson Mnyawami wakati
akizungumza na wanahabari mjini hapa na kusema kuwa endapo serikali
haitowarudisha wanafunzi hao chuoni hapo wapo tayari kufanya maandamano nchi
nzima kwa kushinikiza wanafunzi hao kurudi chuoni kwa sababu kitendo cha
kuwarudisha majumbani ni kuwanyima haki zao za msingi.
Katibu huyo pia ameitaka serikali ya
awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kutafutia ufumbuzi changamoto
mbalimbali katika sekta za umma ili kuepuka kutokea matatizo kama hayo katika
nchi yetu.
Mnyawami alisema kuwa mgogoro wa
walimu na serikali katika chuo kikuu cha Dodoma ni matokeo ya kupuuza madai ya
watumishi wa umma kwa muda mrefu na hivyo kupelekea kuzorotesha utoaji wa
huduma katika sekta za umma,kwani watumishi wa umma wamekuwa wakilalamikia
serikali kwa miaka mingi uboreshwaji wa maslahi yao ikiwamo mishahara
inayokidhi na kuwaboreshea mazingira mazuri ya kazi lakini serikali meonekana
kuziba masikio.
Alisema kuwa Wanafunzi waliofukuzwa
chuo kikuu cha Dodoma ni wanafunzi halai,waliopelekwa na serikali kwa mpango wa
maalumu kwa ajili ya kupunguza adha ya uhaba wa walimu wa sayansi
kwa shule za msingi na sekondari ,serikali ilifanya vyema namna ya kukabiliana
na changamoto hiyo ambapo ilikuja na program ya kuwapeleka walimu waliofaulu
vizuri kidato cha nne upande wa sayansi kwenda kuchukua mafunzo ya
ualimu kwa muda wa miaka mitatu (specia program).
Pia alisema kuwa wanafunzi hao
waliendelea kusoma chini ya udhamini wa bodi ya miopo kwa mujibu wa maelekezo
ya serikali lakini jambo la kushangazwa Mei 25 mwaka huu serikali hiyo ilitoa
tamko kupitia waziri wa elimu Prof.Joyce Ndalichako kuwataka wanafunzi hao
kuondoka kwenye eneo la chuo kwa kile alichodai kwamba kumekuwa na mgomo wa
walimu usiopungua mwezi mmoja mgomo ambao umepelekea walimu kutoingia
madarasani kwa muda mrefu.
Awali akizungumza mwenyekiti wa
chaso Iringa Paschal Sulley alisema kuwa chaso na bavicha Iringa
wamepatwa na wasiwasi mkubwa juu ya utendaji wa mhimili wa bunge katika
utekelezaji wa majukumu yake ya kuisimamia na kuishauri serikali katika awamu
ya tano ambapo imeonekana dhahiri bunge linasimamiwa na serikali.
Sulley alisema kuwa wachaso na
bavicha wamelaani vikali ofisi ya spika kupitia kamati ya bunge haki na
madaraka kuwasimamishwa wabunge wa upinzani kushiriki vikao vya bunge kwani
maamuzi hayo yana hasara nyingi ikiwamo kuwanyima wananchi haki ya
uwakilishi ndani ya bunge hasa katika vikao vya bajeti.
Alisema kuwa kitendo hicho
kinadumaza ukuaji wa demokrasia yetu changa.
Aliongeza kuwa kuondoa sehemu
ya bunge hususani upinzani kunapelekea kulifanya bunge la serikali kukosa
meno kwani hapatakuwapo ka mawazo mbadala katika vikao vya bunge hivyo
kupelekea kupitisha vitu visivyo na tija katika nchi yetu.
0 maoni:
Chapisha Maoni