Posted by Esta Malibiche on Nov3,2016 in NEWS
Katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano kumefanyika jitahada kubwa za kuhakikisha inafufua mashirika yalifikia hali mbaya na kushindwa kutoa huduma ili hatimaye yaanze upya kutoa mchango wa ujenzi wa uchumi nchi. Mojawapo wa Mashirika hayo ni pamoja na Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ambapo kabla ya Rais Magufuli kuingia madarakani lilikuwa na Ndege mmoja tu.
Hatua hiyo ya Rais Magufuli kuamua kununua Ndege mbili aina ya Bombadier Q400 zimesaidia kuimarisha Kampuni hiyo na kurejesha nembo ya Twiga iliyoanza kupotea. Licha ya juhudi hizo na kazi mkubwa aliyoifanya Rais Magufuli ya kutimiza ahadi yake ya kuanza kuijenga upya Kampuni hiyo, wapo baadhi ya wananchi wachache ambavyo wamewakuwa hawana shukurani na kuanza kubeza jitihada hizo.
Ni vema wakumbe ule usemi unaotumiwa na baadhi ya watu kuwa “ Hata mbuyu ulianza kama mchicha” .Kauli hii inadhihirisha kuwa kila jambo uwa na mwanzo wake kwani tokana na dhihaka za baadhi ya watu ambao wamekuwa wakibeza juhudi za Mhe. Rais Magufuli. Ununuzi wa Ndege hizo umesaidia kumeimarisha huduma za usafiri wa anga na kuongeza ushindani katika utoaji wa huduma za anga hapa nchini kati yake na kampuni binafsi za ndege zinazotoa huduma hiyo kwa sasa
Azma hiyo ya Serikali ya kununua ndege mpya imetimiza ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli wa kulifufua tena Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na kulipatia mtaji ili lianze upya kutoa huduma hiyo kwa Watanzania. Akizindua ndege hizo Rais Magufuli alisema kuwa ,ndege hizo zina sifa ya matumizi madogo ya mafuta na ni suluhisho la kupanda kwa bei ya usafiri wa anga nchini na pia zitasaidia kukuza sekta ya utalii nchini.
“Ndege hizi zinatumia wastani wa mafuta ya shilingi milioni moja kutoka hapa hadi Songea, wakati ndege za Jet zinatumia mafuta ya shilingi milioni 28.1 kwa safari kama hiyo,” anasema Mheshimiwa Rais. Ukitaka kujenga nchi yenye uchumi wa kisasa huwezi kujenga bila kuwa na ndege na ukitaka watalii lazima uwe na ndege.
“Tunataka watalii wanaokuja nchini kuja moja kwa moja bila kushuka nchi nyingine ili kuongeza mapato yetu na kukuza utalii duniani na kuwa na ndege nyingi zaidi kama nchi nyingine” anasema Rais Magufuli. Mbali na kuleta ndege hizo, yapo mambo mengi makubwa ambayo Rais Magufuli ameanza kuyatekeleza, aliyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana, hatua ambayo imewavutia watu wengi ndani na nje ya nchi.
Aidha WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa leo alizindua awamu ya kwanza ya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma ili uweze kupokea ndege kubwa za mizigo, abiria na viongozi wa kitaifa na kimataifa. Uzinduzi huo ni miongoni mwa maandalizi ya kutimiza azma ya kuufanya mkoa wa Dodoma kuwa Makao Makuu ya Tanzania. Ujenzi huo umegharimu Sh bilioni 11.5 ambazo ni fedha za ndani na utatoa fursa kwa mashirika ya ndege kuanza huduma Dodoma, ikiwemo ndege ambazo zimenunuliwa na serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana anasema, uzinduzi huo hautaathiri mchakato wa kujenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa eneo la Msalato. “Mchakato wa ujenzi wa uwanja wa ndege Msalato uko pale pale,” anasema Rugimbana na kuongeza kuwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeamua kufanya upanuzi wa uwanja huo ili ndege kubwa zitue mkoani humo.
‘’Wizara ya Ujenzi imeamua kufanya upanuzi wa uwanja wetu wa ndege wa Dodoma ili ndege kubwa ziweze kutua na sisi tunamshukuru Rais kwa kutupa uwanja huo kwani utazidi kufungua fursa katika mkoa wetu,” anaeleza Rugimbana.
0 maoni:
Chapisha Maoni