Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumatano, 30 Novemba 2016

Prof. Ole Gabriel: Sekta ya kilimo mkombozi ajira kwa vijana

Posted by Esta Malibiche on Nov 30,2016 in NEWS
04
Sekta ya kilimo nchini imekuwa mkombozi kwa ajira ya vijana kwa asilimia 81.18 ilikinganishwa na sekta nyingine ambapo idadi ya vijana kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Mkazi ya 2012 wapo vijana milioni 16.2 huku idadi ya vijana wa kike wakiwa milioni 8.3 na wa kiume milioni 7.9 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema hayo leo jijini Mbeya wakati wa mkutano wa wadau wa maendeleo kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 30 ulioitishwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya TechnoServe chini ya Mradi wa Uimarishaji wa Maendeleo ya Vijana Vijijini kupitia Biashara (STRYDE).
Akielezea mgawanyo wa ajira kwa vijana nchini, Prof. Ole Gabriel amesema kuwa sekta ya Umma nchini inaajiri vijana 188,000, sekta binafsi vijana 1,027,000 wakati vijana wanaojiajiri ni 1,100,000.
Prof. Ole Gabriel amesema kuwa taasisi ya TechnoServe kupitia mradi wake wa STRYDE imekuja na mbinu ambayo imewapa kipaumbele vijana wengi na kuwapa elimu ya kujitambua ili wabadili utamaduni wao wa kufikiri waweze kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo katika maeneo yao.
01
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na wadau wa maendeleo (hawapo pichani) jijini Mbeya wakati wa mkutano wa  kuwajengea uwezo vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 30 ulioitishwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya TechnoServe chini ya Mradi wa Uimarishaji wa Maendeleo ya Vijana Vijijini kupitia Biashara (STRYDE).
Katika kuinua vijana kichumi, Prof. Ole Gabriel amesema kuwa mwanadamu ana sehemu kuu mbili ambazo ni sehemu inayoonekana (mwili) na sehemu isiyoonekana inayoshughulika na fikra ambayo inamsaidia mwanadamu katika kuboresha maisha yake pamoja na jamii yake.
“Shughulikeni na sehemu isiyoonekana ya vinjna ndiyo muhimu, mkifanya hayo mtawakomboa vijana na taifa” alisema Prof. Ole Gabriel.
Kufuatia sehemu hizo kuu za mwanadamu, taasisi ya TechnoServe imekuwa msatari wa mbele katika kuhakikisha inamjengea uwezo vijana kujua na kutumia fursa walizo nazo kwa kubadili fikra zao katika kufanyakazi.
Prof. Ole Gabriel amewapongeza TechnoServe kupitia mradi wake wa STRYDE kwa kuwainua vijana kifikra na kubadilisha mfumo wao wa maisha ambalo hilo ni jambo la kuigwa na kujivunia.
02
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi. Mariam Mtunguja akimkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati wa mkutano ulioitishwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya TechnoServe chini ya Mradi wa Uimarishaji wa Maendeleo ya Vijana Vijijini kupitia Biashara (STRYDE).
Vilevile ametumia fursa hiyo ya kukutana na vijana kwa kumpongeza kijana Clementina Jairo mwenye umri wa miaka 23 kutoka Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kwa kuwa balozi mzuri wa mradi huo kwa kufanya kazi za ujariamali kwa ujasiri mkubwa ambapo alianza kilimo cha kibiashara kwa mtaji wa sh.2000 na sasa anamiliki mtaji wa akiba ya sh.500,000 katika Benki ya NMB.
Akitoa taarifa ya taasisi yake kwa Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mkazi wa TechnoServe nchini Bi. Alexandra Mandelbaum amesema kuwa taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali katika kutatua tatizo la ajira kwa vijana kwa kuwajengea uwezo kifikra ili waweze kuendesha maisha yao ambapo kwa sasa wanatoa mafunzo kwa vijana katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Bi. Alexandra amesema kuwa TechnoServe inatarajia kuwafikia vijana 15,430 ifikapo 2019 ambapo mradi wa kuwajengea uwezo vijana kiuchumi unatekeleza kwa miaka mitano kuanzia mwaka 2014.
03
Mkurugenzi Mkazi wa TechnoServe nchini Bi. Alexandra Mandelbaum akitoa taarifa ya taasisi yake na kuahidi wataendelea kushirikiana na Serikali katika kutatua tatizo la ajira kwa vijana kwa kuwajengea uwezo kifikra ili waweze kuendesha maisha yao jijini Mbeya.
Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi. Mariam Mtunguja amkakikishia Mkurugenzi Mkazi wa TechnoServe nchini kuwa Serikali ya mkoa wa Mbeya itaendelea kuwapa ushirikiano ili kuhakikisha mkoa huo unapambana na adui umasikini kwa kubadilisha fikra za vijana katika maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Aidha, Bi Mariam ameongeza kuwa wataweka mazingira wezeshi ya kijinsia na kijamii kwa vijana ili waweze kuzitumia fursa zilizopo katika kujiongezea kipato.
Kwa upande wake kijana Clementina Jairo ambaye ni mnufaika wa mafunzo ya STRYDE amesema kuwa ndoto yake ni kuwa mjasiriamali mkubwa anatarajia kufanya biashara ya pembejeo za kilimo na kuwa mkulima wa kilimo cha kisasa.
Mradi wa Uimarishaji wa Maendeleo ya Vijana Vijijini kupitia Biashara (STRYDE) unatekelezwa katika nchi nne za Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda chini ya ufadhili wa MasterCard Foundation.
04
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akimpongeza kumpongeza kijana Clementina Jairo mwenye umri wa miaka 23 kutoka Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kwa kunufaika kwa Mradi wa Uimarishaji wa Maendeleo ya Vijana Vijijini kupitia Biashara (STRYDE) ambapo ameanza kilimo cha kibiashara kwa mtaji wa sh.2000 na sasa anamiliki mtaji wa akiba ya sh.500,000 katika Benki ya NMB.
05
Mkurugenzi Mkazi wa TechnoServe nchini Bi. Alexandra Mandelbaum (kushoto) akimpongeza Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) mara baada ya kutoa hutuba wakati wa mkutano jijini Mbeya.
06
Kijana Clementina Jairo kutoka Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya akitoa ushuhuda namna alivyonufaika na Mradi wa Uimarishaji wa Maendeleo ya Vijana Vijijini kupitia Biashara (STRYDE) ambapo ameanza kilimo cha kibiashara kwa mtaji wa sh.2000 na sasa anamiliki mtaji wa akiba ya sh.500,000 katika Benki ya NMB.
07
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja mara baada mkutano na wadau wa Mradi wa Uimarishaji wa Maendeleo ya Vijana Vijijini kupitia Biashara (STRYDE) jijini Mbeya.(Picha na Eleuteri Mangi,- WHUSM, Mbeya)

KIWANGO CHA UFAULU MTIHANI WA DARASA LA SABA 2016 MKOA WA IRINGA CHAONGEZEKA NA KUFIKIA ASILIMIA 99.5

Posted by Esta Malibiche on Nov 30 ,2016 In NEWS
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu akizungumza na wandishi wa Habari[Hawapo pichani]katika kikao cha kutangaza matokeo ya Mtihani wa darasa la saba mwaka 2016 kilichofanyika ukumbi wa Siasa ni Kilimo Halmashauri ya wilaya ya Iringa,Mkoani Iringa.


Na Esta Malibiche

Iringa

Kiwango cha ufaulu wa mitihani ya kumaliza Elimu ya Msingi 2016 Mkoani Iringa kimeongezeka kutoka wastani wa 82.8% mwaka 2015  hadi kufikia 99.5% mwaka 2016.

Akizungumza na wandishi wa Habari katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo uliiopo katika Halmashauri ya Wialaya ya Iringa,Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu alisema

Ayubu lisema ongezeko hilo ni mafanikio makubwa ambayo yameufanya mkoa kushika nafasi ya 3 kitaifa kati ya mikoa 26 ya Tanzania bara.

‘’’’Ongezeko la ufaulu linaleta changamoto mpya ambayo kuwa na madarasa na madawati ya kutosha kwa idadi ya wanafunzi wote.’’’Alisema Ayubu

Akichanganua matokeo hayo alisema mwaka 2016 mkoa ulikuwa na watahiniwa 21,270 waliosajiliwa kufanya mtihani,  ambapo waliofanya mtihani walikuwa watahiniwa 21,177 ikiwa ni sawa na 99.5% namwa 2015 waliofaulu mtihani ni watahiniwa 17,587  sawa na 82.8%.

‘’’’Halmashauri ya mji wa Mafinga imeweza  kuongeza kiwango cha ufaulu ambapo Mafinga imeweza kushika nafasi ya nne kitaifa wakati Kilolo imeongeza ufaulu kutoka kwa 13%, Wilaya ya Iringa kwa 12%.’’’’alisema Ayubu.

Kwa upande wake Afisa elimu wa mkoa Richard Mfugale alisema mwaka huu hakukuwa na tuhuma zozote za udanganyifu wa mitihani kama ilivyotokea miaka ya nyuma.

Mfugale alisema kuwa wanafunzi 413 hawakuweza kufanya mtihani kwa sababu mbalimbali ikiwemo utoro, vifo, ugonwa , mimba na kuhama.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Stevin Mhapa alisema wamefanikiwa kuongeza kiwango cha ufaulu kutokana na kufuata ushauri uliotolewa kwenye kikao kama hicho kilichopita sambamba na kufanya tathimini za mara kwa mara.

“SHULE ZA MSINGI 88 ZA HALMASHAURI YA BUHINGWE KIGOMA ZAMUENZI BABA WA TAIFA “

Posted by Esta Malibiche on Nov. 30,2016 in NEWS


kigoz1
Matofali yaliyofyatuliwa na wanafunzi Mradi wa Elimu ya Kujitegemea yanatumika kujengea vyoo na madarasa pale penye upungufu wa vyumba vya madarasa na Vyoo (Picha na Bizei)
kigoz2
Baadhi ya wanafunzi wakila chakula shuleni.
kigoz3
Matofali yaliyofyatuliwa na wanafunzi Mradi wa Elimu ya Kujitegemea yanatumika kujengea vyoo na madarasa pale penye upungufu wa vyumba vya madarasa na Vyoo (Picha na Bizei)
……………………………………………………………………..
Judith Mhina – MAELEZO
Shule za Msingi za Serikali katika Halmashauri ya Buhigwe zipo 88 zamuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa kutekeleza kwa vitendo miradi  102 ya  Elimu ya Kujitegemea.
Hayo yamesemwa na  Waratibu Elimu Kata 5 wa Halmashauri hiyo, waliokuwa wakihudhuria  Mafunzo ya siku mbili yaliyoendeshwa na  Mpango wa Kuinua  Elimu Tanzania EQUIP – TZ, Mwezi Novemba mwaka huu, katika Ukumbi wa VanCity katika Halmashauri ya Wilaya ya  Kasulu Kigoma.
Kiongozi wa Waratibu Kata hao Mwalimu Maxmillan Joseph alisema:” Halmashauri ya  Buhigwe imefanikiwa kwa  kiasi kikubwa kuwa na         miradi ya elimu ya kujitegemea na kupunguza dhana ya  utegemezi kwa serikali kwa asilimia mia moja”.
Mwalimu Maxmillan aliongeza :” Mfano zoezi zima la utengenezaji wa  madawati katika Mkoa wa Kigoma, mbao zilizo nyingi zimetoka katika miradi ya kujitegemea ya Shule za Msingi za Buhigwe, hili ni jambo la kujivunia.”
Miradi ya shule hizo za Msingi ina lengo la kuwaandaa wahitimu katika shule hizo kujengewa uwezo wa kujitegemea kuilingana na mazingira ya mahali walipo na kuanzisha shughuli zao mara baada ya kuhitimu darasa la saba.
Aidha, baadhi ya miradi hiyo inahusu shughuli za Kilimo, Ufugaji, Misitu, Mazingira, Ufyatuaji na uchomaji matofali na biashara ya vifaa vya elimu Mfano shule ya Msingi Mwayaya ipo Kata ya Mwayaya ina mradi wa duka la vifaa vya elimu vya  rejareja, Shule  ya Gwimbogo  kupanda miche ya mikaratusi robo ekari,  shule ya Kibila mradi wa migomba nusu ekari, Shule ya  Manyovu ufugaji wa kuku 30 na mbuzi 3 majike
Kata ya Muhinda shule ya Ruhuba A  robo ekari bustani ya mbogamboga Ruhuba B, kilimo cha Migomba nusu ekari,  shule ya  Nyarubo ina  mradi  wa ufugaji mbuzi jike 1,  shule Muhinda kuku 10 wa asili, shule ya Kigaraga uboreshaji shamba la kahawa ekari
nusu. Kata ya Buhigwe shule ya Buhigwe mradi wa migomba robo hekari, shule ya Kavomo shamba la miti robo ekari na shamba la mbegu za majani ya malisho ya wanyama robo ekari. Shule ya Nyankoronko kilimo cha mahindi nusu ekari, shule ya Mulera migomba nusu ekari, na mananasi robo ekari shule ya Nyamiti kilimo cha mananasi nusu ekari, shule ya Kafene mananasi nusu ekari.
Shule Kavomo mbogamboga za kupanga kwenye maji yaani saladi na mradi wa ng’ombe 2 majike wa maziwa shule ya Rusaba upandaji mti 200 robo ekari Rusaba B upandaji miti ya kahawa 200 robo ekari, shule ya Mpanzigo uendelezaji shamba la kahawa nusu ekari. Nyarabingo upandaji wamiche ya kahawa 150  robo ekari. Shule ya Kibwiga kilimo cha migomba ekari shule ya Kiyanga kilimo cha mananasi, nusu ekari shule ya Mikanda duka la vifaa vya elimu Nyaregano kuku wa mayai  100 shule ya Kilalama ufugaji wa kuku wa asili 40.
Pamoja na miradi yote hiyo ya shule kiwango cha elimu cha Halmashauri ya Buhigwe kimepanda kutoka nafasi ya 6  ya wilaya mpaka 4. Kama ifuatavyo,  Mwaka 2013 ilikuwa nafasi ya 6,  2014 ilikuwa 5,  2015   5  2016 4 ki Mkoa
Itakumbukwa Muasisi wa Taifa hili Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Azimio la Arusha ambalo lilitoa muongozo wa Elimu ya Kujitegemea. Katika Awamu ya Mwalimu na dhana ya kujitegemea ilianza kujengwa kwa mtoto kuanzia shule ya Msingi, Sekondari, Vyuo vya Ufundi, Vyuo  Vikuu  na  sehemu za kazi kila Afisa au Mtumishi wa Serikali alitakiwa kuwa mfano katika kufanya mradi au shghuli yoyote ya kujitegemea ili mradi isijihusishe na matumizi mabaya ya fedha za umma au ya nafasi yako kazini.
Dhana hii ya Mwalimu Nyerere, iliweza kujenga Taifa la watu wenye uwezo wa kumudu maisha yao ya kila siku bila kufikiri kuna baba, mama, mjomba au shangazi wa kukuhudumia kama kijana. Tafiti mbalimbali zinaonyesha Vijana wengi wa Tanzania hawawezi kubuni, kutafakari muelekeo wa maisha yake binafsi na kupelekea lawama zote kuiangukia Serikali kwamba haitoi ajira kwa vijana.
Pamoja na juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano  ya kuandaa nafasi nyingi za uongozi kwa vijana na kuweka mazingira mazuri kwa vijana kujiajiri, bado tatizo ni kubwa  la vijana kupenda kufanya shughuli ambazi  sio endelevu na ambazo haziwezi kuwajengea uimara wa kumudu maisha yao ya kila siku.
Wilaya ya Buhigwe ni mfano wa kuigwa na Tanzania nzima kwani shule za Msingi 88 zote zinamiradi ya kujitengemea, jambo la kusikitisha Mkoa wa Kigoma Halmashauri zote zilizobakia hazina miradi ya elimu ya kujitegemea kama Buhigwe. Hakika Buhigwe mnastahili pongezi , ushauri wangu ni vema mkahakikisha Mkoa wa Kigoma wote unakuwa mfano bora kwa Watanzania kwani ardhi ipo yenye rutuba haihitaji mbolea kutukana na asili yake ya udongo uliotokana na Volkano na uwepo wa bonde la ufa la Ziwa Tanganyika.  volkano

UFAULU DARASA LA SABA WAPANDA MKOA WA SINGIDA; ELFU KUMI NA NNE KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2017.

Posted by Esta Malibiche on NOV 30,2016 In NEWS


mkonooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
Kiwango cha ufaulu wa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi Mkoani Singida kimepanda kutoka wastani wa asilimia 58.41 mpaka asilimia 69.25 ikiwa ni ongezeko la asilimia 11 huku wanafunzi 14,759 wakichaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari kwa kidato cha kwanza kwa mwaka 2017.
Buhacha Baltazar Kichinda akiongoza kikao cha uteuzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2017 kama Kaimu Katibu Tawala Mkoa na mwenyekiti wa kikao hicho amesema mkoa umefaulisha wavulana 6,852 na wasichana7,907 huku akiwapongeza waalimu wote kwa bidii ya ufundishaji iliyopelekea mkoa wa singida kushika nafasi ya 12 kati ya Mikao 26 ya tanzania bara.
Kichinda ameipongeza halmashauri ya Itigi kwa kushika nafasi ya kwanza kati ya halmasahuri saba za mkoa wa singida na ya 38 kitaifa kati ya halmashauri 186 za Tanzania bara huku ikifaulisha kwa asilimia 80.41. Aidha amewatia moyo halmasahuri ya Mkalama kwa ufaulu hafifu wa 57.51 na kuwa nafasi ya 155  kitaifa.
Kichinda ameongeza kuwa kwa sasa kila Mkurugenzi wa halmasahuri anapaswa kukaa na wadau wake wa elimu ili kupanga mikakati ya kuboresha zaidi elimu, amesema lengo kubwa kwa sasa ni kuhakikisha kila mwanafunzi aliyefaulu anajiunga na kidato cha kwanza na kumaliza elimu ya sekondari.
Amesema sekta ya elimu inachangamoto mbalimbali ikiwemo utoro wa walimu na wananfunzi, miundombinu ya vyumba vya madarasa kutotosheleza mahitaji halisi, upungufu wa waalimu, uhaba wa nyumba za walimu pamoja na waalimu wenyewe kuwa wachache tofauti na mahitaji halisi hivyo amewata wadau wa elimu kujipanga kutatua changamoto hizo na sio kusubiria serikali kuu kufanya kila kitu.
Aidha kichinda amesema kuwepo na utaratibu wa kuwapongeza waalimu hasa kwenye shule zilizofanya vizuri ili iwe motisha kwa kazi wanayoifanya huku akiitangaza shule ya msingi Utaho ya halmasahuri ya Ikungi kuwa ya kwanza kimkoa kwa shule zenye wananfunzi zaidi ya 40 na shule ya msingi Aghondi ya Itigi kuwa ya kwanza kimkoa kwa shule ambazo zina wanafunzi chini ya 40.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo amesema ili kuboresha elimu mkoani Singida msisitizo uwepo wa kuhakikisha wananfunzi wote wanapata chakula shuleni ili waweze kusikiliza kwa umakini mzuri.
Tarimo ameongeza kuwa wazazi wanapaswa kutambua kuwa elimu bila malipo haiwaondolei wajibu wao kama wazazi wa kuhakikisha wanafunzi wanakula, wanalala na kuvaa hivyo hivyo watakaposhirikishwa katika kuchangia chakula, ujenzi wa mabweni au shuguli za elimu wajitoe kwani wamiliki wa shule ni wazazi.
Amesema utaratibu wa kufanya ukaguzi ili kuwatambua waalimu watoro au wazembe ufanyike katika halmashauri zote na kwa viongozi wote wanaotembelea vijijini bila ya kusubiri ziara maalumu ya ukaguzi na kuongeza kuwa hali hiyo itawaongezea umakini waalimu katika kutekeleza majukumu yao lakini pia watendaji watabaini changamoto za waalimu na shule na kuzitatua kwa uharaka.

MATUKIO KATIKA PICHA KILELE CHA MAONYESHO YA UTALII KITAIFA MKOANI IRINGA

Posted by Esta Malibiche on Nov 30,2016 In NEWS

Wananchi  mjini  Iringa  wakitembelea banda la Iringa  Foods & Logistic Ltd watengenezaji wa pipi aina mbali mbali  pamoja na Snacks zenye  ubora  zaidi  jivunie bidhaa bora kutoka  Iringa  tembelea  maonyesho ya  utalii Tanzania katika  viwanja vya Kichangani mjini Iringa


Chuo  Kikuu Huria  Cha  Tanzania  tawi la Iringa   wakitoa maelekezo  mbali mbali katika banda  lao  lililopo  viwanja vya maonyesho ya Utalii Tanzania kichangani mjini Iringa

UN NA EU YAWANOA MABALOZI 50 WA MALENGO YA DUNIA IRINGA

 
Posted by Esta Malibiche on Nov 30,2016 in NEWS
 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mpango wa misaada ya maendeleo UNDAP II 2016-2021 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa, Dr. Cephas Mgimwa alipomtembelea ofisini kwake mjini Iringa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akifafanua jambo juu ya ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya Maendeleo 2016-2021 (UNDAP II) kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa, Dr. Cephas Mgimwa alipomtembelea ofisini kwake mjini Iringa
Mwanasheria wa Chuo Kikuu cha Ruaha Iringa, Martin Noel akiwa ameongozana Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano chuoni hapo sambamba Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendesha semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia.

Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro akielezea fursa za ufadhili wa masomo nje ya nchi katika tovuti ya Umoja wa Ulaya Tanzania wakati wa semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia (Global Goals Champions) huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia iliyofadhiliwa na EU.
Mkufunzi wa Malengo ya Dunia ambaye pia ni Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akiwapiga msasa vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia (Global Goals Champions) huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia kwenye semina hiyo iliyofadhiliwa na EU.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro akiwa amejumuika na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha wakati wa semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana 50 ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia (Global Goals Champions) huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia ambapo semina hiyo imefadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) nchini.
Pichani juu na chini ni vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha walioshiriki semina maalum ya kuwa mabalozi wa malengo ya dunia (Global Goals Champions) iliyoandaliwa na UN na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) mjini Iringa.
 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) akimkabidhi cheti Rais wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa Athman Waziri aliyehitimu kuwa balozi wa Malengo ya Dunia (Global Goals Champion).
Picha juu na chini Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea na zoezi la kutunuku vyeti kwa mabalozi wa malengo ya dunia kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha.


Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Malengo ya Dunia (Global Goals Champions) baada ya kuhitimisha semina maalum iliyoshirikisha vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Mwanasheria wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa, Martin Noel baada ya kuhitimisha semina ya malengo ya dunia mjini Iringa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Afisa Habari wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU), Muazarau Matola
Baadhi ya Global Goals Champions katika picha ya kumbukumbu na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu.
Mkufunzi wa Malengo ya Dunia ambaye pia ni Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akibadilishana mawazo na wahitimu wa semina malengo ya dunia (Global Goals Champions) mara baada ya kuhitimisha semina hiyo iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Ruaha mjini Iringa ambapo imefadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).