Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo( kushoto) akiwa na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku,( kulia)
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo( kushoto) akiwa pamoja na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku( kulia ) pamoja na watendaji wa Taasisi zilizochini ya Wizara ya Nishati wakati wa kikao na ujumbe kutoka nchini Afrika Kusini waliotaka kufahamu zaidi fursa za uwekezaji nchini Tanzania.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo( kulia) akiwa na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku( katikati) pamoja na Patiwe Makoena Afisa anayeshughulikia masuala ya siasa katika ubalozi wa Afrika Kusini.( kushoto) wakati wa Kikao na Waziri wa Nishati nishati na madini, pamoja na watendaji wa taasisi zilizochini ya wizara hiyo hawapo pichani.
Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa milango ya uwekezaji iko wazi kwa
Mataifa yote duniani yenye nia thabiti ya kufanya hivyo nchini Tanzania.
Profesa Muhongo alisema hayo
jijini Dar Es Salaam wakati wa kikao chake na Balozi wa Afrika Kusini
hapa nchini,Thami Mseleku, ambaye alifika Ofisi za Wizara ya Nishati na
Madini kufahamu zaidi fursa za uwekezaji kwa ajili ya manufaa ya Kampuni
za uwekezaji za Afrika Kusini .
Katika kikao hicho, Profesa
Muhongo alimueleza Balozi Mseleku kuwa Tanzania ina fusra nyingi za
uwekezaji katika masuala ya Nishati na kutaja maeneo hayo kuwa ni pamoja
na makaa ya mawe, Nishati jadidifu,Upepo,mawimbi ya bahari pamoja na
umeme wa jua.
Aidha Profesa Muhongo alimueleza
Balozi Mseleku kuwa Kampuni za uwekezaji kutoka Afrika Kusini zimekuwa
zikifanya vizuri katika Sekta ya Madini hasa katika kulipa mirabaha na
tozo mbalimbali za zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini.
Vilevile Waziri wa Nishati na
Madini alimsisitiza Balozi huyo wa Afrika Kusini kusini kuwekeza katika
sekta ya gesi ambayo tayari inapatikana hapa nchini ili kuzalisha umeme
kwa kuwa Tanzania inahitaji umeme mwingi, wa uhakika na wa kutosha.
Profesa Muhongo alieleza kuwa
Tanzania inatarajia kufikia katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025
utakaotokana na uwepo wa nishati ya umeme ya kutosha nchini, pia tayari
imesaini Mpango wa Umoja wa Mataifa unaoelekeza kila mtu kupata huduma
ya umeme ifikapo mwaka 2030 unaofahamika kama ” SE4ALL” Nishati Endelevu
kwa wote.
Kwa upande wake Balozi Afrika
Kusini hapa nchini, Thami Mseleku,alisema kuwa inchi yake ipo tayari
kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo nishati ya gesi, mafuta na
makaa ya mawe na kwamba nchi hiyo inauzoefu zaidi katika uwekezaji wa
nishati ya makaa ya mawe. Balozi huyo wa Afrika Kusini katika Mkutano
huo aliambatana na Afisa anayeshughulikia masuala ya siasa, Patiwe
Makoena
0 maoni:
Chapisha Maoni