Jumanne, 22 Machi 2016

Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo aongoza kuaga mwili wa marehem Mwanjisi




 
katibu mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(mwenye miwani) akiwa amebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu mkuu wa zamani Wizara ya Habari Marehemu Frank P. Mwanjisi  aliyefariki jijini Dar es Salaam.Marehemu amesafirishwa leo kwenda mbeya kwa ajili ya mazishi.



Mchungaji kutoka kanisa la KKKT usharika wa kariakoo akiendesha misa ya kumuombea marehemu Frank Mwanjisi  ambaye aliwahi kushika wadhifa wa katibu mkuu katika wizara ya Habari.
Picha na Daudi Manongi-WHUSM


 Katibu mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akimpa pole Elifasi Mwanjisi ambaye ni mdogo wa marehemu  Frank Mwanjisi aliyekuwa katibu mkuu wa zamani Wizara ya Habari leo jijini Dar es Salaam.



Mtoto wa marehemu ,Bw Charles Mwanjisi(mwenye t-shirt nyeusi) akizungumza jambo na mkurugenzi msaidizi-MAELEZO Bw.Raphael Hokororo wakati wa misa.

Katibu mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa katibu mkuu wa zamani wa wizara ya Habari Marehemu Frank Mwanjisi aliyefariki jijini Dar es Salaam.




 

0 maoni:

Chapisha Maoni