WATU WATATU WALIKUTWA WAMEUAWA NA
MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO MEXICO
GUEST HOUSE AMBAKO WALIFIKIA WAKIANDIKA KWENYE KITABU CHA KULALA WAGENI
KUWA WANATOKEA SONGEA.
MAREHEMU WALITAMBULIKA KWA MAJINA
WALIOJIANDIKISHA KWENYE KITABU CHA WAGENI 1. MARIAM HASSAN, MGONI,
MFANYABIASHARA ALIANDIKA KWENYE KITABU CHA WAGENI KUWA ANATOKEA
SONGEA ALIKODI CHUMBA NAMBA 15
AKIWA NA MWANAUME MMOJA AMBAYE HAKUANDIKA TAARIFA ZAKE KWENYE KITABU CHA
WAGENI 2. ABBAS YASINI, MZARAMU, MFANYABIASHARA, AMBAYE PIA ALIANDIKA
KWENYE KITABU CHA WAGENI KUWA ANATOKEA SONGEA NA ALIFIKIA CHUMBA NAMBA
14 NA 3. TATIZO ADAM, MKINGA, MKULIMA AMBAYE ALIANDIKA KUWA ANATOKEA
SONGEA NA ALIKODI CHUMBA NAMBA 103.
AWALI MNAMO TAREHE 19.03.2016
MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI INADAIWA KUWA HAPO KATIKA NYUMBA YA KULALA
WAGENI IITWAYO MEXICO GUEST HOUSE WALIFIKA WATU WANNE AMBAO KATI YAO
WATATU WALIKUWA WANAUME NA MMOJA ALIKUWA NI MWANAMKE. WAGENI HAO
WALICHUKUA VYUMBA VITATU, CHUMBA NAMBA 15 ALICHUKUA MAREHEMU MARIAM
HASSAN AKIWA NA MWANAUME AMBAYE HAKUANDIKA TAARIFA ZAKE KWENYE KITABU
CHA WAGENI.
AIDHA MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI
WAGENI HAO WALIONEKANA WAKITOKA NA BAADAE WALIRUDI NA KISHA KUKAA
CHUMBANI KWA MARIAM HASSAN WAKIWA WANAONGEA NA KUNYWA VINYWAJI.
MNAMO TAREHE 20.03.2016 MAJIRA YA
SAA 07:30 ASUBUHI, MTU MMOJA AMBAYE ANAISHI JIRANI NA NYUMBA HIYO YA
WAGENI ALIONA MOSHI UKITOKA KWENYE CHUMBA NAMBA 15 AMBACHO ALIFIKIA
MAREHEMU MARIAM HASSAN NA NDIPO ALITOA TAARIFA KWA WAHUDUMU WA NYUMBA
HIYO YA KULALA WAGENI NA KISHA KWENDA KUKAGUA NA KUKUTA MIILI YA
MAREHEMU IKIWA IMENYONGWA NA BAADAE KUCHOMWA MOTO NDANI YA CHUMBA HICHO.
HATA HIVYO INADAIWA MAPEMA
ASUBUHI TAREHE 20.03.2016, MWANAUME AMBAYE HAKUANDIKA TAARIFA ZAKE
KATIKA KITABU CHA WAGENI NA ALILALA CHUMBA NAMBA 15 CHA MAREHEMU MARIAM
HASSAN, ALIONDOKA AKIWA AMEBEBA NDOO NDOGO NA BEGI DOGO NA KUDAI KUWA
YEYE ANAONDOKA [ANASAFIRI] ILA WENZAKE AMEWAACHA WAMEPUMZIKA.
CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO
HAKIJAFAHAMIKA. MMILIKI WA GUEST HIYO BWANA SPIRIAN BONIPHACE MTENGELA,
ANASHIKILIWA KWA MAHOJIANO KUHUSIANA NA TUKIO HILO. UPELELEZI UNAENDELEA
IKIWA NI PAMOJA NA KUMTAFUTA MTUHUMIWA ALIYEHUSIKA KATIKA TUKIO HILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA. MIILI YA MAREHEMU
IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA – KYELA KWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA
KWA UTAMBUZI TOKA KWA NDUGU NA JAMAA.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAMSHIKILIA MHAMIAJI HARAMU MMOJA RAIA WA NCHINI RWANDA ALIYEFAHAMIKA
KWA JINA LA TUNSUMILE CLAUD [19] AKIWA AMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
20.03.2016 MAJIRA YA SAA 09:30 ASUBUHI HUKO NSALAGA, KATA YA NSALAGA,
TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KISHERIA
ZINAFANYIKA ILI AKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI.
WATU WAWILI WOTE WAKAZI WA
IYELA JIJINI MBEYA WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. SHADRACK MOTON [25] NA
2. FRANK YOHANA [21] WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
WAKIWA NA BHANGI KETE 18 NA MISOKOTO 12.
WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO
TAREHE 201.03.2016 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA
HUKO MAENEO YA IYELA, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA
MBEYA. WATUHUMIWA WALIKAMATWA ANA BHANGI HIYO AMBAYO WALIKUWA WAMEIFICHA
KWENYE MFUKO WA RAMBO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUTOA
TAARIFA ZA MTU/WATU AU KIKUNDI CHA WATU WANAOJIHUSISHA NA
UINGIZAJI/USAMBAZAJI NA UUZAJI WA DAWA ZA KULEVYA ILI WAKAMATWE.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 maoni:
Chapisha Maoni