Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakiendelea na utaratibu wa kusaini kitabu cha wageni.
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakielekea mwenye ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kupewa taarifa na Kaimu Mkurugenzi wa mfuko huo Bw. Michael Muhando wa kwanza kulia. |
Baadhi ya wakurugenzi wa vitengo NHIF wakifuatilia mambo kadhaa wakati wa uwasilishaji wa ripoti hiyo mbele ya Makamti ya Bunge Maendeleo ya Jamii, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Rehani Athumani na Ali Othman Mkurugenzi wa TEHAMA NHIF.
Mjumbe wa kamati Mbunge wa Buchosa Mh. Dk Charles Tizema akitoa mchango wake katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk . Mpoki Ulisubisya akifafanua jambo mbele ya kamati hiyo huku wabunge wakifuatilia.
Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Mhando akitoa ufafanuzi wa mambo kadhaa yaliyojadiliwa na kamati hiyo pamoja na uongozi wa NHIF.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua kituo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu kilichoanzishwa kwa ajili ya kuwafanya wateja kupata taarifa mbalimbali kuhusu mfuko huo bila kulazimika kufika ofisini.
0 maoni:
Chapisha Maoni