Jumatatu, 21 Machi 2016

WAZIRI NAPE AZINDUA MSIMU MPYA WA MASHINDANO YA UREMBO YA MISS TANZANIA 2016








Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwasili kwenye hoteli ya Ramada Resort akiambatana na Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia).



 Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga akitoa mukhtasari wa mashindano hayo kwa mwaka huu 2016 kwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kushoto). Kushoto ni Mlezi wa kamati ya Miss Tanzania ambaye pia ni Balozi wa Tanzania nchini Botswana, Mh. Emmanuel Ole Naiko na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akifurahi jambo na mmoja wa wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania.
 Wajumbe wa kamati ya mashindano ya Miss Tanzania 2016 wakitambulishwa mbele ya mgeni rasmi Waziri Nape Nnauye (hayupo pichani).
 Msanii wa Bongo Flava, Linah Sanga katika ubora wake.
 Kutoka kushoto ni Miss Tanzania 1998, Basila Mwanukuzi, Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu, Miss Tanzania 2008, Nasreen Kareem pamoja na Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima wakipozi katika picha ya pamoja kwenye uzinduzi wa Msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016.
 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kulia) pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza wakishuhudia burudani mbalimbali zilizokuwa zikiendelea ukumbini hapo.
 aziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiendelea na mazungumzo na waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania na Wajumbe wa kamati hiyo kabla ya kuelekea kwenye uzinduzi rasmi.
 Kikundi cha sanaa cha Wanne Star kikitoa burudani kwenye hafla ya uzinduzi wa Msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Ramada Resort ya jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza wakishuhudia uzinduzi wa nembo mpya ya mashindano ya Miss Tanzania 2016 yaliyobeba kauli mbiu ya “Mrembo na Mazingira Safi”
IMG_7035
IMG_6959
Pichani juu na chini ni wadau wa tasnia ya urembo na wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa Msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016.
Miss Tanzania 2016
Linah Sanga
Msanii wa Bongo flava, Linah Sanga na ma-dancers wake wakitoa burudani kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016.
Linah Sanga
Msanii wa Bongo Flava, Linah Sanga katika ubora wake.

0 maoni:

Chapisha Maoni