Baadhi ya vijana walikuwa wakitumia dawa za kulevya kwa sasa wameacha |
Mlezi wa kituo hicho cha Iringa Sober Hous Bw Godwin Msillu kushoto akiwa na baadhi ya vijana waliokuwa watumiaji wa dawa za kulevya ambao wanaishi kituoni hapo |
Shadrack John ambae ni anaishi kituo cha Iringa Sober House aliyetoka mkoa wa Arusha akijisomea Biblia baada ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya |
Na MatukiodaimaBlog.
KAMANDA wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa Bw Salim Asas ameunga mkono kwa vitendo mapambano ya vita dhidi ya madawa ya kulevya nchini yaliyoanzishwa na Rais Dr John Magufuli kwa kusaidia uanzishwaji wa kituo cha kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya mkoani hapa.
KAMANDA wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa Bw Salim Asas ameunga mkono kwa vitendo mapambano ya vita dhidi ya madawa ya kulevya nchini yaliyoanzishwa na Rais Dr John Magufuli kwa kusaidia uanzishwaji wa kituo cha kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya mkoani hapa.
Bw Asas
ambae wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu alipata kuweka bayana
mkakati wake wa kusaidia vijana walioathiriwa na matumizi ya madawa
ya kulevya ameungana na kituo cha Iringa Sober House kilichopo
Semtema katika Manispaa ya Iringa kuwasaidia vijana hao ambao afya
zao zimeathiriwa na madawa ya kulevya kwa kuwakusana na kuwapatia
tiba.
Akizungumza na
mtandao wa Kali ya Habari Dr Alli Ngalla ambae ni Mkurugenzi wa
NGOs ya Foundation for ellevition of drug eddiction anda sufferings
(FADAS) wameanzisha kituo cha kutoa huduma kwa waathirika wa madawa
ya kulevya cha Iringa Sober House ambacho kimeanza kufanya kazi
chini ya ufadhili mkubwa wa Bw Asas .
Alisema kuwa
kituo kituo hicho toka kimefunguliwa kina zaidi ya mwezi mmoja
ambapo jumla ya wategemezi 7 ambao wanahudumiwa katika kituo hicho
pamoja na wasimamizi watatu ambao pia walikuwa ni watumiaji wa dawa
za kulevya ambao kwa sasa waliacha .
Kwa kweli kuendelea kwa kituo hiki kumechangiwa kwa karibu
na Salim Asas ambae amekuwa bega kwa bega kuona vijana walioathirika
na madawa ya kulevya wanasaidiwa na anachofanya salim pia ni
kumuunga mkono Rais Dr Magufuli ambae ametangaza vita dhidi ya
madawa ya kulevya ……hivyo bado tunaomba wadau wengine
kujitokeza kusaidia mapambano haya ya kunusuru afya za vijana wetu
“alisema Dr Ngalla.
Kuwa
lengo la kituo kuweza kuwahudumia waathirika wa madawa ya
kulevya kutoka mikoa mbali mbali nchini hasa wamelenga
kuwafikia vijana wa mkoa wa Mbeya, Njombe , Ruvuma na Iringa japo
tafiti zinaonyesha mkoa wa Mbeya ndio unaongoza kwa matumizi ya
madawa ya kulevya
Msimamizi
wa kituo hicho Bw Godwin Msillu alisema kuwa mkakati wa
kuanzisha kituo hicho ulitokana na mkakati wa NGOS ya
FADAS ambao walikuja na mpango wa kuanzisha kituo hicho .
Alisema
kuwa kati ya waathirika wa dawa za kulevya ambao wapo kituoni
hapo baadhi yao ni kutoka mkoa wa Arusha na kuwa kumekuwepo
na mafanikio makubwa kwa walengwa hao afya zao kuanza kuimarika na
hivyo kuwataka vijana wengine walioathirika na dawa za kulevya
kutosita kufika kituoni hapo ili kusaidiwa zaidi.
Akizungumza
kwa niaba ya wenzake walioathirika na madawa ya kulevya Bw
Shadrack John alisema kuwa amepata kufika mkoani Arusha kuja
kupatiwa huduma hiyo na kuwa kwa sasa hali yake inaendelea vizuri
zaidi.
0 maoni:
Chapisha Maoni