MWIGULU NCHEMBA KUHAMISHA UFUGAJI KUTOKA UFUGAJI HOLELA KWENDA UFUGAJI WA VITARU
Picha/Maelezo na Festo Sanga
Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh:Mwigulu Nchemba akimuangalia mmoja wadume
la ng'ombe anayetumika kuzalisha Mitamba kwenye kitaru namba 9 shamba
la kitengule-Karagwe.Baadhi
ya ng'ombe waliopo kitaru namba 9 shamba la kitengule ambapo kwenye
block hii moja kuna Ng'ombe zaidi ya 800 wanaolishwa na kuhudumiwa
vizuri na mmiliki wa kitaru hiki.Ng'ombe
wakitoka kuogeshwa kwaajili ya kuua baadhi ya wadudu kama kupe
wanaopendelea kukaa kwenye mwili wa ng'ombe.Hili ni moja ya josho la
kisasa ndani ya kitaru namba 9.
Kufuatia ziara ya waziri mkuu,Mh:Kassim
Majaliwa ndani ya mkoa wa Kagera akiwa ameambatana na waziri wa
Kilimo,Mifugo na Uvuvi pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani,Ziara
hiyo imekuja na maagizo kadhaa ikiwamo wamiliki wote wa vitaru kwenye
ranchi za Taifa ambao hawajaziendeleza waziachie mara moja na maeneo
hayo yagawiwe upya,Waziri Mkuu ameagiza pia kwa wamiliki wa vitaaru
ambao sio watanzania wajisalimishe au waondoke kwenye vitaru hivyo kabla
hatua kali hazijaanza kuchukuliwa.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi
Mh:Mwigulu Nchemba akiwa na timu yake ya wataalamu wameshaanza kupitia
vitaru vyote "blocks" na wamiliki wake ikiwepo pia idadinya mifugo kwa
kila block,Hii leo Mwigulu Ncheba amekutana na wamiliki wa vitaru kwenye
shamba la Kitangile-Karagwe na kuagiza wamiliki wote ambao
hawajaendeleza maeneo wanayoyamiliki yanachukuliwa na serikali kwaajili
ya kuwapatia watanzania wenye uwezo wa kuziendesha.
Mwigulu Nchemba ameagiza pia wamiliki wa
vitaru kuacha mchezo wa kukodisha na kuingiza mifugo kutoka kwa
wafugaji haramu wa nchi jirani,kitendo hicho ni kosa na yeyote
atakayebainika anakwenda jela na adhabu kali itafuta.
Mbali na vitaru hivyo,Waziri Mkuu
akishirikiana na waziri wa kilimo wameagiza ofisi ya mkuu wa mkoa wa
kagera kuondoa wavamizi wote kwenye pori tengefu ya serikali kabla hatua
zingine zinazofuata kuanza kutekelezwa.
Kupitia uwekezaji mzuri kwenye kitaru
namba 9 cha shamba la Kitengule,Mwigulu Nchemba ametoa rai kwa wafugaji
wote nchini kuanza kujipanga kufuga kwa mfumo wa vitaru ili kuachana na
ufugaji holela unaopelekea migogoro mbalimbali na wakulima.
0 maoni:
Chapisha Maoni