Mshindi chama cha Republican Florida na Ohio hukabidhiwa wajumbe wote
Donald
Trump amepiga hatua katika kukaribia kutwaa tiketi ya kuwania urais
kupitia chama cha Republican nchini Marekani baada ya kushinda mchujo
majimbo matatu makubwa, likiwemo jimbo la Florida.
Bilionea huyo kutoka New York ameshinda majimbo ya Illinois na North Carolina.
Hata hivyo ameshindwa na John Kasich jimbo la Ohio.
Mgombea
anayeongoza chama cha Democratic Hillary Clinton naye amepanua uongozi
wake kwa kupata ushindi majimbo ya Florida, Ohio, Illinois na North
Carolina.
Marco
Rubio, mmoja wa waliotarajiwa kutoa ushindani kwa Trump katika chama cha
Republican amejiondoa baada ya kushindwa na Trump katika jimbo lake la
nyumbani la Florida.
Majimbo matano makubwa, Florida, Missouri, North Carolina, Ohio, Missouri na Illinois, yalifanya mchujo Jumanne.
Trump amemsifu Rubio"Lazima tuunganishe chama,” amesema Bw Trump akihutubu Palm Beach, Florida, baada ya kupata ushindi.
Anatumai kwamba ushindi huo utamfungulia njia ya kupeperusha bendera ya chama cha Republican.
John Kasich hata hivyo ameshinda jimbo lake la kwanza tangu mchujo kuanza, jimbo la Ohio ambako yeye ndiye gavana.
Akihutubu
baada ya ushindi, Bw Kasich amesema anataka kuweka “mazingira ya kubuni
nafasi” kwa vizazi vijavyo na pia akampongeza Bw Rubio kwa kampeni
yake.
Bw Rubio ametangaza kujiondoa kwake kwenye kinyang’anyiro katika mkutano wa kampeni mjini Miami baada ya kushindwa Florida.
Amesema Marekani imo kwenye dhoruba ya kisiasa na kwamba wapiga kura wamekasirika na kutamauka.
0 maoni:
Chapisha Maoni