Alhamisi, 17 Machi 2016

WANANCHI LUMULI WAMLILIA WAZIRI WA KILIMO KUHUSU PEMBEJEO



Diwani wa kata ya Lumuli katika Jimbo la Kalenga Halmashauri ya wilaya ya Iringa,mkoani hapa Charles Lutego ameitaka serikali  kwa kupitia waziri aliyepewa dhamana ya kilimo mh.Mwigulu Nchemba kupunguza bei za mbolea ili wakulima hasa wa kipato cha  chini waweze kumudu na kununua.
Kauli hiyo ameitoa leo [jana]hii kufuatia malalamiko ya  wakulima  kuhusu uhaba wa pembejeo na kucheleweshwa kupatikana kwa pembejeo hizo alisema kuwa kumekuwa na udanganyifu mkubwa kutokana na badhi ya mawakala kutokuwa waaminifu kujipandishia bei za vocha kinyume na taratibu ya serikali na kusababisha wakulima wenye kipato cha chini kushindwa
Lutego alisema kutokana na hujuma hizo ameitaka serikali  isimamie upatikanaji wa mbolea kwa wingi na kwa bei nafuu na ihakikishe mnyonge ambae ni mkulima hasa wa kijijini anaipata kwa wakati unaotakiwa ili aweze kunufaika na kilimo hicho.
‘’’Wakulima wamekuwa wakilalamika kuhusu ucheleweshwaji wa mbolea, na mawakala kuwasainisha wakulima mapema kabla mbolea haijafika  hali inayosababisha udanganyifu mkubwa kwa wakulima napengine kutoletwa kabisa vijijini kutokana na uzembe wa mawakala wakati serikali,huku serikali ikitambua kuwa mbolea zinawafikia mapema wakulima na kwa wakati’’’’alisema
Akizungumzia changamoto hiyo amesema baadhi ya mawakala  wamekuwa  wakiwasainisha wakulima vocha kabla ya kufika na kusababisha udanganyifu mkubwa kwa wanyonge
Kwa upande wake waziri wa kilomo,mifugo na uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na Rdio maria kwa njia ya simu amesema,serikali imejipanga kuhakikisha wakulima wanaondokana na kero hizo nchini ili kilimo kiweze kuwakomboa


Mwigulu amesema wizara  yake inalengo la kuona  sekta ya  kilimo inaboreshwa nchini na kuhakikisha  wakulima  wanapanda mbegu  bora kwa wakati katika maeneo yao na mbolea inawafikia kwa wakati ili waweze kunufaika na kilimo kwa kupata mazoa mengi.
‘’Nimesikia kilio cha wakulima wangu kuhusu mawakala na pembejea kutowafikia kwa wakati naahidi kutekeleza nitalishugulikia kwa kusimamia  mimi mwenyewe na kuhakikisha nalitatua na ninapenda niwahakikishie wananchi  kuwa changamoto hiyo  haitatokea tena‘’alisema Nchemba.

‘’’Sitokuwa tayari kumvumilia mtu yeyote atakaezembea kwa makusudi katika wizara yangu ikiwa nipamoja na hili la wakulima wa lumuli na jimbo la kalenga kwa ujumla kukosa pembejeo kwa makusu ikiwa ni pamoja na kuwacheleweshea huku wakitozwa bei tofauti na serikali ilivyopangwa’’’’.
Aidha Waziri Mwigulu amewataka wananchi  kuachana na kilimo cha mazoea kwa kupanda mazao ya aina moja kila mwaka hali inayopelekea uahaba wa chakula endapo zao hilo halitatoa mazao mengi na aliwataka kubadilisha mazao kulingana na msimu na hali ya hewa ya eneo husika ili mashamba yao yaweze kuzalisha rutba ya kutosha.

‘’’Serikali inampango wa kutoa elimu kwa wananchi na kuhamasisha kuhusu zao la alizeti na mtama ili wakulima waweze kubadili kilimo kuendana na ukanda wao,lengo ni kutaka mkulima asitegemee zao moja’’’’alisema

Akizungumzia kuhusu kilimo cha  zao la alizeti alisema kuwa,zao hilo lina fursa kubwa katika soko hapa nchini,kutokana na asilimia kubwa ya wananchi hupenda kutumia mafuta ya alizeti kwa sababu hayana athari kiafya,hivyo wananchi wanayofursa ya kujikita kwenye kilimo cha zao hilo .


0 maoni:

Chapisha Maoni