Mbunge wa Kilolo Bw Venance Mwamoto akijaribu kutwanga kwa kutumia kinu.
MGANGA wa Zahanati ya Ibumu wilaya ya Kilolo aliyekataliwa hivi karibuni mbele ya mbunge wa Kilolo Bw Venance Mwamoto kwa madai ya kuwanyanyasa azidi kukwaza wananchi adaiwa kutishia kuwashughulikia wote waliomchongea ,wananchi wapanga kuandamana
Wananchi walipanga kuandamana kwenda Zahanati hapo kwa ajili ya kumwondoa kwa nguvu mganga huyo baada ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilolo kupuuza utekelezaji wa maombi ya wananchi kutoka mganga huyo kuondolewa katika zahanati hiyo kwa kudai ni jipu .
Wamesema mganga huyo huyo Gasalamwike Mgongolwa hawamtaki katika kata hiyo kutokana na kufanya kazi kwa mazoea na kuwa na visasi kwa wagonjwa na mbali ya kulalamika mbele ya mbunge ila bado mganga huyo yupo na anaendelea kutishia maisha ya wagonjwa .
Tayari mbunge wa Kilolo Bw Mwamoto ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya kilolo kufika kesho Alhamis katika Zahanati hiyo ili kuchunguza na kuchukua hatua ya kumwamisha ama ya kinidhamu kwa mganga huyo .
mbunge Mwamoto alisema suala la mganga huyo amefikisha kwa mwajiri wake ambae ni mkurugenzi wa halmashauri ya Kilolo kwani yeye hana uwezo wa kumfukuza ama kumhamisha hivyo kuwataka wananchi kuwa watulivu .
Akizungumza kwa njia ya simu mganga Mgogolwa alidai kuwa tuhuma dhidi yake hazina ukweli bali yeye anafanya kazi kwa kujituma zaidi na wapo watu ambao wanaendekeza majungu
Amesema yeye kila siku anafika kazini asubuhi saa 1:30 na kutoka saa 9 Alasiri saa kwa mujibu wa taratibu za kazi.
0 maoni:
Chapisha Maoni