Jumanne, 22 Machi 2016

MAMIA WAJITOKEZA KUUAGA MWILI WA BIBI JOSEPHINE SIMON MSHUBUSI, MWILI WASAFIRISHWA KWENDA BUKOBA KWA MAZISHI




Mkurugenzi wa Mabibo Beer, James Lugemarila, (kulia), akziungumza wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Bibi Josephine Simon Mshumbusi kwenye Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania, KKKT, Kijitonyama jijini Dar es Salaam Machi 20, 2016.

 Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda Bukoba mkoani Kagera kwa mazishi yatakayofanyika Jumanne Machi 22, 2016. 
(Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said.
MWILI wa marehemu bibi Josephine K. Simon Mushumbusi umeagwa leoMachi 20, 2016 kwenye
kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania, KKKT, Kijitonyama jijini Dar es Sala na tayari umesafirishwa kwenda kijiji ni kwake, Kashura mkoani Kagera kwa mazishi.
Mrehemu Josephine ambaye alifariki Machi 18, 2016 baada ya kusumbuliwa na malaria kali alizaliwa Mei 2, 1931 kwenye kijiji cha Kashura mkoani Kagera na ameacha watoto kadhaa., .
Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu ilianza majira ya mchana na mamia ya wakazi wa jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake walifika kwenye ibada hiyo, motto mkubwa wa marehemu, ambaye ni Mfanyakazi wa UTT-PID, Euginia Simon, amesema mazishi ya
mama yake yatafanyika Jumanne Machi 22, 2016 kijijini alikozaliwa. Bwana alitoa bwana alitwaa na jina lake lihimidiwe.



 

 Mwili wa marehemu ukiwa kanisani kwa Ibada



Mbunge wa mafinga mjini[ccm] COSATO CHUMI akishiriki Ibada ya kumuaga marehemu Josephin simoni

0 maoni:

Chapisha Maoni