Ijumaa, 18 Machi 2016

Angelina Mabula awaita Watanzania Tamasha la Pasaka

Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Ilemela, Angelina Mabula ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Mwanza na maeneo ya karibu kujitokeza kwa wingi kwa sababu ya unyeti wa Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Machi 27 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Akizungumza jana, Mabula alisema Tamasha la Pasaka ni la Watanzania wote, lakini mwaka huu wamepata bahati ya kufikiwa na ujumbe wa neno la Mungu ambao utakemea maovu kama mauaji ya vikongwe na walemavu wa ngozi ‘albino’.“Binaadam anatakiwa kubaki na heshima yake, kwani hakuna maisha bora ambayo yanatokana na kuwaua na kuwakata viungo wenzao, si ubinaadam kabisa tunatakiwa tumrudie Mungu kwani ndio kimbilio,” alisema 

.Mabula alisema Tamasha la Pasaka limebeba ujumbe wa neno la Mungu hivyo ni nafasi kwa wakazi wa Ilemela na maeneo ya jirani na hata mikoa mingine kujitokeza kwa wingi kufanikisha tamasha hilo.Aidha Mabula alisema thamani ya Tamasha la Pasaka ni kubwa hivyo Watanzania ni nafasi yetu Watanzania kumfikishia Mungu sala zetu.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama  alisema maandalizi ya kuelekea tamasha hilo yanaendelea vizuri, hivyo wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wakae mkao wa kula.
Msama alisema Tamasha la Pasaka litaanza Machi 26 mkoani Geita na kufuatiwa jijini Mwanza Machi 27 na kumalizia Machi 28 mjini Kahama kwenye uwanja  wa Taifa mkoani Shinyanga.
Msama alitaja viingilio katika tamasha hilo ni shilingi 5000 kwa wakubwa na watoto shilingi 2000, naye alitumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kuimuimbia na kumtukuza Mungu.

0 maoni:

Chapisha Maoni