Mtakumbuka kwamba mnamo tarehe 13 Oktoba
2015, nilitangaza kuihama CCM na kurejesha kadi yangu ya uanachama
kwenye ofisi ya CCM Kata ya Mikocheni. Nilitoa maelezo kwanini niliamua
kujiondoa CCM (maelezo hayo pia niliyabandika katika ukurasa wangu wa
facebook). Nilieleza kwamba CCM imepoteza mwelekeo kwa kuamua kumnyima
haki ya kugombea mcha mungu Edwad Lowasa. Nikasema Edwad Lowasa ndiye
chaguo la wana-CCM na ndiye chaguo la Watanzania. Nikasema nitakuwa
mnafiki nikiendelea kubaki CCM huku naamini Edwad Lowasa anafaa kuwa
Rais kuliko John Pombe Magufuli.
Baada ya miezi miwili ya uongozi wa
Magufuli nataka niseme nilikosea sana. Nililewa mahaba ya Lowasa,
nililewa ahadi ya Lowasa kunipa uwaziri wa mambo ya Nje. Niliamini
mafuriko ya Lowasa ambayo yakanifanya niamini kabisa anachukua nchi.
Tulikubaliana na wenzangu kwamba wiki mbili za mwisho tuihame CCM kwa
wimbi kubwa ili kuitikisa na kuitoa madarakani. Lakini baadhi wakaogopa
na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana vyeo.
Leo natangaza kurudi CCM kwasababu
nimeona kazi nzuri ya Magufuli. Nimefanya kosa kubwa katika siasa ambalo
nawasihi vijana kwenye siasa wasifanye. Nilihama kwa kwasababu ya mtu
(Lowassa). Nimerudi kwasababu ya mtu (Magufuli). Nataka niwaahidi kwamba
CCM ikiweka mtu hovyo baada ya Magufuli, sitahama. Usemi wa CCM kwamba
Chama Kwanza, Mtu Baadaye sasa ndio nauona maana yake. Niliwalaumu CCM
kwa kumuacha Lowassa lakini sikujua kwamba CCM ina uwezo wa miujiza wa
kuibua jembe bora linaloitwa Magufuli.
Naomba mnisamehe kwa kulifanya jambo
langu la kujitoa CCM na kurudi CCM kuwa jambo la kitaifa ukizingatia
kwamba sikuwa na nafasi yoyote ya uongozi wa CCM wakati nahama na pia
sijawahi kuwa hata Mjumbe wa NEC ya CCM na nilikuwa nje ya ulingo wa
siasa za CCM kwa miaka 20. Niliamua kulifanya jambo kubwa ili kumsaidia
Lowassa. Na sasa nimeamua kulifanya jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa
niko naye kwasababu sitaki shughuli zangu na za washirika wangu
zikwamishwe na Serikali kwasababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia
swahiba wangu.
Naomba radhi kwa familia ya baba wa
taifa Mwalimu Nyerere kwa kuitumia kisiasa siku aliyokufa (tar 14
Octoba) na kutumia msiba wake kutoa kauli za kisiasa zidi ya chama chake
alichokiunda na ambacho hadi anakufa alikuwa mwanachama.
Wananchi wote tumuombee Magufuli na tumsaidie kwani tumepata nyerere mpya.
Mungu Ibariki Tanzania
mungu Ibariki Afrika
0 maoni:
Chapisha Maoni