Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi. Irina Bokova.
Shakespeare,
mwandishi maarufu kutoka Uingereza aliyefariki yapata miaka 400
iliyopita, aliandika katika tamthilia yake inayojulikana kama “A
Midsummer Night’s Dream” kuwa, “Jicho la mshairi, hutazama kwa umakini
na undani, kutoka mbinguni hadi duniani, na duniani hadi mbinguni. Na
kama vitu vya kufikirika vusivyofahika vinavyoumbika katika mawazo,
ndivyo kalamu ya mshairi inavyogeuza mawazo hayo kuwa katika maumbo
yasiyoweza kudhaniwa”
Kwa
kuwatambua na kuwaheshimu wanaume na wanawake, ambao chombo chao pekee
ni uhuru wa kujieleza, watu wanaofikiria na kuchukua hatua, UNESCO
inatambua thamani ya ushairi kama ishara ya ubunifu wa mwanadamu. Kwa
kutoa umbo na maneno kwa mambo ambayo katika hali ya kawaida hayakuwa
nayo, kama vile uzuri usiopimika unaotuzunguka na mateso na taabu kubwa
za dunia, mashairi yanachangia upanuzi wa ubinadamu wetu, kwa kusaidia
kuongeza nguvu za ubinadamu wetu, mshikamano na kujitambua.
Sauti
zinazobeba ushairi husaidia kukuza upana na utofauti wa lugha na uhuru
wa kujieleza. Sauti hizi hushiriki katika jitihada za kimataifa kuelekea
elimu ya kisanii na usambazaji wa utamaduni. Wakati mwingine, neno la
kwanza la shairi latosha kabisa kurejesha kujiamini pale mtu anapokuwa
anakabiliwa na upinzani na kupelekea kuiona tena njia ya matumaini pale
unapopambana na unyama. Katika zama hizi za teknolojia na uharaka wa
maisha ya kisasa, ushairi hufunya nafasi kwa ajili ya uhuru na
kuvinjari, hali iliyo ndani ya utu wa mwanadamu. Kutoka Arirang za huko
Korea hadi Pirekua za Mexico, nyimbo za Hudhud za jamii ya watu wa
Ifugao, Alardah za Saudi Arabia, Koroghlu za jamii ya watu wa
Turkmenistan na maeneo ya Iran na Afghanistan, na Aitysh za watu wa
Kyrgyz, kila utamaduni una aina ya sanaa yake ya ushairi inaoutumia
kupeleka na kusambaza maarifa, maadili ya kijamii na kiutamaduni na
kumbukumbu za pamoja, ambayo huimarisha kuheshimiana, mshikamano wa
kijamii na kutafuta amani.
Leo
hii, nawapongeza washairi, wasanii, waghani, na wale wote ambao sauti
zao, bila ya wao wenyewe kujulikana, wamejitoa, kwa na kupitia ushairi,
kutoa masomo katika hali ya taswira au ya uwazi, katika bustani au
katika mitaa. Ninatoa wito kwa nchi wanachama wote wa UNESCO kuunga
mkono juhudi hizi za ushairi, ambao una uwezo wa kutukusanya pamoja,
bila kujali asili au imani, kwa lile lililo hasa katika kiini cha
ubinadamu
0 maoni:
Chapisha Maoni