Watu 31
wamefariki baada ya mashambulio kutekelezwa katika uwanja wa ndege wa
Zaventem na kituo cha treni cha Maelbeek mjini Brussels.
Waziri wa
afya wa Ubelgiji amesema watu 11 walifariki na wengine 81 kujeruhiwa
baada ya milipuko miwili kutokea uwanja wa ndege wa Zaventem, nje kidogo
ya mji wa Brussels.
Meya wa Brussels amesema watu 20 walifariki Maelbeek.
Kundi linalojiita Islamic State limedai kutekeleza mashambulio hayo
Waziri
Mkuu wa Ufaransa Francois Hollande amelaani mashambulio hayo mjini
Brussels na kusema ni kama mashambulio yaliyolenga bara lote la Ulaya.
Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel amesema hatua zaidi zimechukuliwa kuimarisha usalama mpakani.Milipuko
hiyo imetokea siku nne tu baada ya kukamatwa kwa mshukiwa mkuu wa
mashambulio ya Paris ya mwaka jana ambayo yalisababisha vifo vya watu
130.
Abdeslam alikamatwa Ijumaa katika mtaa mmoja wa Brussels.
Uwanja wa
ndege wa Zaventem unapatikana kilomita 11 kaskazini mashariki mwa
Brussels na ulihudumia abiria zaidi ya 23 milioni mwaka jana.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni