Vijana
nchini wametakiwa kuachana na tabia ya
kutumika vibaya na wanasiasa kwa kuunda
makundi ya kuwakashifu viongozi
yasiyokuwa na maslai yao,bali wajiunge katika vikundi vya ujasiliamali
ili waweze kunufaina na mikopo imnayotolewa na serikali ili waweze kunufaika nayo kwa kufanya
biashara ili kujikwamua kimaisha
Kauli hiyo
imetolewa na katibu wa umoja wa vijana ccm mkoa wa Iringa Abdulikarim Halamga
leo wakati akizungumza na KALI YA HABARI ofisini kwake na kusema
kuwa vijana wengi wanakosa fursa za maendeleo ikiwa pamoja na kupoteza haki yao ya msingi kutokana na
kujikita zaidi kwenye makundi ya kisiasa yasiyoleta manufaa kwao na Taifa kwa
ujumla
Halamga
alisema vijana `ndiyo rasilimali ya Taifa
lakini imekuwa ni kinyume kutokana na wao kupoteza muda mwingi kutumika
viabaya kuwachafua viongozi wa serikali na chama kwa ujumla kwa kupitia makundi yao na kujisahau kuwa wanahitaji kujitafutia mkate wa kila siku na
kuboresha maisha yao.
Hivi karibuni serikali itaanza kutekeleza ahadi ya kugawa fedha mil.50 kwa kila kijiji
ikiwa ni utekelezaji wa ialani ya chama cha mapinduzi ccm aliyoahidi Mh. Rais
wakati akifanya kampeni za uchaguzi mkuu uliopita,vijana wanatakiwa
kuchangamkia fursa hiyo kwa kujiunga kwenye vikundi vya mikopo.
Kutokana na
hali hiyo kwa mkoa wangu wa Iringa nimeamua kufanya ziara kila wilaya
kuzungumza na viongozi wa umoja wa vijana katika kata zao wakiwemo makatibu na
wenyeviti ili waweze kuachana na siasa za makundi yasiyo na tija na wajikite
kwenye siasa za kiuchumi kwa kuchangamkia fursa zinazotolewa na
serikali’’’’alisema
Aidha
alisema ziara yake ameianzia wilaya ya Iringa mijini ambapo alizungumza na baraza la vijana akiwashukuru kwa kukipa
heshima chama cha mapinduzi kuhakikisha kinabaki madarakani.
‘’’’Nimeamua
kuwashukuru wananchi na kutoa zawadi ya mashine ya kuchapa kila wilaya ili umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi
ccm uweze kuimalika kwa kufanya kazi na kufuata misingi ya chama
inavyosema.ikiwa nipamoja na kuwaasa vijana kuchangamkia fersa zinazotolewa na
serikali kwa utekelezaji wa ilani ya
chama cha mapinduzi ccm’’’alisema
0 maoni:
Chapisha Maoni