Peneza alisema kuwa anaamini watu
wakimpenda Mungu wataacha kufanya mauaji ya vikongwe na albino na watu
wa kawaida, kwani mkoa huo unaongoza kwa mauaji ya aina hii.
Alisema Tamasha hilo ni msaada
mkubwa kwa mkoa huo kwani litahamasisha na kupinga mauaji huku
akisisitiza kuwa kampuni ya Msama ambayo inasifika kusaidia jamii
anaiomba pia iwafikie hata watoto wa mitaani wa mkoa wa Geita.
“Tunamshukuru Msama na kamati
yake kwani Tamasha linaweza kuwa msaada mkubwa kwa mkoa wetu mauaji
yamezidi si kwa walemavu wa ngozi na vikongwe hata watu wa kawaida
wanauwawa kwa mapanga na vitu vingine” alisema Peneza.
Alitolea mfano wa mauaji ya
aliyekuwa Mwenyekiti wa mkoa wa Chadema, Alfonce Mawazo aliyeuwawa kwa
kukatwakatwa mapanga hivyo kupitia tamasha la pasaka litawaasa waache
mauaji.
“Kupitia hili Tamasha naamini
wataacha vitendo hivyo kwa sababu Mungu anasema tusiue, mpende mwenzio,
kwa hiyo mimi nadhani tamasha hili liwe la kihistoria kwa ajili ya
kuwataka na kumrudia mungu,” anasema.
Peneza alisema asiwe Msama tu hata asasi, kampuni na wadau mbalimbali wajitokeze kupinga mauaji kwani hilo ni janga la kitaifa.
0 maoni:
Chapisha Maoni