Alhamisi, 17 Machi 2016

Simba kususa Ligi Kuu

Haji Manara msemaji wa timu ya mpira ya  Simba akizungumza na wandishi wa habari  jijini Dar es salaam

CLABU ya Simba imesema baada ya kumalizika kwa mchezo wao ujao dhidi ya Coastal Union, hawatacheza michezo iliyobaki hadi timu za Yanga na Azam zitakapomaliza viporo vyao.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, msemaji wa Simba, Haji Manara alisema anadhani timu hizo zimekuwa zikipangiwa matokeo ndio maana zimekuwa zikibadilishiwa ratiba mara kwa mara.
Alisema watasubiri timu hizo zimalize viporo na kulingana ndipo waendelee na ratiba ya ligi. “Kwa nini Yanga haikucheza wiki hii kupunguza viporo vyake, mbona Asernal ilicheza juzi na Watfod na leo (jana) walicheza na Barcelona tena mechi kubwa?
Yanga na Azam ni akina nani, tunaonewa,” alisema. Manara alikwenda mbali zaidi na kusema inawezekana Bodi ya Ligi inashinikizwa kubadili ratiba ndio maana inashindwa kutekeleza majukumu yake vizuri na kwamba kuna mazingira yanayojengwa kuwakwamisha.
Yanga na Azam wana viporo kutokana na kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika na ile ya Shirikisho. Timu hizo zimekuwa zikiomba mabadiliko ya ratiba ya ligi kwa ajili ya kufanya maandalizi mazuri ya michezo hiyo.
Timu hizo kila moja ina viporo viwili na huenda wiki ijayo ikashindwa kucheza kutokana na maandalizi ya timu ya Taifa ’Taifa Stars’ inayotarajia kucheza mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa Afrika wiki ijayo nchini Chad.
Msemaji huyo alitoa lawama kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwamba kuna malalamiko yao mengi dhidi ya wapinzani wao Yanga, lakini hayafanyiwi kazi. Alisema kuwa kinachofuata ni wao kupeleka barua ya malalamiko kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ili kusikiliza kilio chao kwani TFF wameshindwa kuwasikiliz

0 maoni:

Chapisha Maoni