Na Anitha Jonas – MAELEZO
………………………………………………….
Kaimu Mkurugenzi Jiji la Dar es
Salaam Bi. Sara Yohana amemtanganza Mhe. Isaya Chacha Diwani wa Kata ya
Vijibweni (CHADEMA) kutoka Manispaa ya Temeke kuwa Meya Mpya wa Jiji
hilo.
Kaimu Mkurugenzi huyo alimtangaza
Isaya kuwa mshindi mara baada ya uchaguzi huo kufanyika leo jijini Dar
es Salaam ambapo mshindi alipata kwa kura 84 dhidi ya mgombea kupitia
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw.Yenga Yusuph ambaye alipata kura 67 wakati
kura 7 ziliharibika katika uchaguzi huo.
“Tunawashuruku wapiga kura wote
mlioshiriki zoezi hili la upigaji kura kwa utulivu bila vurugu na kuweza
kufanikisha mpaka kumpata Meya wa Jiji hili” alisema Bi Yohana.
Kwa upande wa mshindi wa Kiti cha
Meya wa Jiji Mhe. Chacha aliwashukuru wapiga kura wake wa kata ya
Vijibweni kwa kumchagua kuwa Diwani pamoja uongozi wa chama chake
kukubali kumpa nafasi ya kugombea kiti hicho.
“Nimejipanga kuleta maendeleo
katika sekta ya elimu pamoja na kupambana na kero ya foleni katika jiji
letu na nitahakikisha wananchi wote maskini wanafaidika na mapato ya
jiji hili ikiwemo kuendeleza miundombinu mbalimbali ,”alisema Chacha.
Aidha, Mwenyekiti wa CHADEMA taifa
Bw.Freeman Mbowe alisema idadi ya wapiga kura tu inaonyesha wazi kuwa
ushindi wa kiti hicho cha Meya ni lazima uchukuliwe na CHADEMA sababu
madiwani wengi wa Mkoa wa Dar es Salaam wanatoka katika chama hicho.
0 maoni:
Chapisha Maoni