04:54
WANANCHI wa Wilaya ya
Mwanga mkoani Kilimanjaro, wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiunga
katika mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) hatua ambayo itasaidia kuboresha
huduma za afya, ikiwa ni pamoja na kupunguza tatizo la upungufu wa dawa
na vifaa tiba kwenye hospitali, vituo vya afya na hata zahanati.
Rai hiyo ilitolewa jana
na Mkuu wa Wilaya hiyo, Shaibu Ndemanga, wakati akizindua kampeni za
uhamasishaji wananchi kujiunga na CHF, uliofanyika katika kata ya Kifula
wilayani humo, ambapo alisema Bima ya Afya ni muhimu sana katika
kupunguza gharama za matibabu na kutatua changamoto ya vifaa tiba kwenye
hospitali na vituo vya afya.
Ndemanga alisema,
wananchi wengi wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa dawa na vifaa tiba
katika maeneo ya kutolea huduma za afya ikiwemo hospitali na kushindwa
kutambua kuwa, chanzo cha tatizo hilo ni wao kutojiunga kwa wingi na
Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Ndugu zangu wananchi,
naomba mjitokeze kwa wingi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ili
kujihakikishia kupata huduma bora za afya, pindi mtakapougua na tambueni
kuwa kujiunga kwenu kwa wingi kutapunguza tatizo la ukosefu wa dawa na
vifaa tiba katika hospitali zetu, vituo vya afya na hata Zahanati,î
alisema Ndemanga.
Alisema tafiti
zinaonyesha kuwa, watu wengi wamekuwa wakijikuta katika wakati mgumu wa
kimaisha pindi wanapougua, kutokana na kukosa fedha za matibabu, hivyo
ni vyema wakajiunga na CHF kabla hawajaugua, ili kujiwekea uhakika wa
kupata matibabu na huduma bora za afya.
Alisema asilimia 37.8
ya wananchi wa Wilaya hiyo ndiyo wamejiunga na mfuko wa afya ya jamii na
kwamba wamejiwekea malengo ifikapo Juni 30 mwaka huu 2016, wawe
wamefikia asilimia 50 na kwamba hilo litafanikiwa endapo viongozi
kuanzia ngazi za vitongoji, vijiji na hata kata watashirikiana
kikamilifu kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko huo.
Naye Meneja wa Mfuko wa
Afya ya Jamii (CHF) kutoka makao makuu Slivery Mgonza, alisema katika
kukabiliana na changamoto ya upungufu wa vifaa tiba na dawa, ipo
changamoto ya rasilimali fedha na kwamba ili kukabiliana na changamoto
hiyo kuna haja ya wananchi kujiunga kwa wingi katika mfuko huo wa CHF.
Alisema lengo la
serikali kwa sasa ni kuboresha huduma za afya na kuhakikisha huduma
zinazotolewa ni bora na si bora huduma na kwamba mpango wa kuchangia
huduma za matibabu kabla ya kuugua ni wa msingi sana.
"Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya umedhamiria kutoa huduma bora za afya na hakuna mwananchi
ambaye atachangia katika CHF na kukosa dawa, lakini pia naomba mfahamu
kuwa tuko kwenye mchakato wa kuboresha mfuko huu ili mgonjwa aweze
kwenda hadi mkoani pindi inapolazimik
0 maoni:
Chapisha Maoni