Musukuma:Tamasha la Pasaka lipige vita mauaji ya vikongwe, albino
……………………………………….
Na Mwandishi Wetu
……………………………………….
MBUNGE wa Geita vijijini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Joseph Kasheku Musukuma
Amewahi kutamka bungeni kuwa
vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi wamekuwa wanauawa wanne kwa wiki
kitu ambacho ni kibaya na sio cha kibinaadamu.
Mbunge huyo alisema kuwa kutokana
na kampuni ya Msama kutambua umuhimu wake wana kila sababu ya kuwaunga
mkono na angependa kuona wananchi wanajitokeza kwa wingi katika tamasha
hilo ili kuzungumza na Mungu kupitia waimbaji na viongozi wa dini
katika tamasha hilo litakalofanyika mikoa ya Kanda ya ziwa.
Alisema hiyo ni kama dawa ambayo
imekuja kutibu tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na
vikongwe hivyo anaamini kuwa nguvu za Tamasha hilo wataweza kusonga
mbele.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya
maandalizi ya Tamasha la Pasaka Alex Msama alisema tamasha hilo
litafanyika mkoani Geita kuanzia Machi 26 kwenye ukumbi wa Desire, Machi
27 kwenye uwanja wa CCM Kirumba na Machi 28 litafanyika uwanja wa Taifa
wilayani Kahama.
Waimbaji mbalimbali wamethibitisha kushiriki katika tamasha hilo
0 maoni:
Chapisha Maoni