Alhamisi, 17 Machi 2016

ZIMBABWE YAPIGA MARUFUKU NDOA ZA WATOTO


Sasa itakuwa kosa kubwa kwa wazazi kuanzisha mazungumzo ya ndoa kwa niaba ya mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18 nchini Zimbabwe.
Makamu wa rais wa taifa hilo Emmerson Mnangagwa amesema katika gazeti la serikali la Helrald wazazxi pia watapigwa marufuku kukubali mahari kabla ya mtoto wao kutimia miaka 18.
Serikali imesema kuwa haitangojea uamuzi wa kikatiba utakaopiga marufuku ndoa za mapema miongoni mwa watoto na tayari imebaini vipengee ambavyo vinapaswa kubadilishwa alisema makamu huyo wa rais.
Kipengee katika sheria ya ndoa kinachoruhusu ndoa za watoto baada ya idhini walindi wao ama mahakama itabadilishwa.
Sheria hiyo ya kimila ambayo ilikuwa haizungumzi kuhusu ndoa za watoto,itabadilishwa ili kushirikisha kipengee inayopinga ndoa hizo bwana Mnangagwa aliongezea.

0 maoni:

Chapisha Maoni