Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumanne, 29 Machi 2016

IDADI YA VIFO AJALI YA BASI IRINGA YAFIKIA 6 MAJERUHI 36,ASAS ATOA MSAADA WA DAWA KWA MAJERUHI WOTE

IDADI YA VIFO AJALI YA BASI IRINGA YAFIKIA 6 MAJERUHI 36,ASAS ATOA MSAADA WA DAWA KWA MAJERUHI WOTE


Majeruhi  wa ajali   Bi Janeth Raia  wa Rwanda  akiwa na mtoto  Ishine Jasmin ambae  pia  Raia wa Rwanda aliyepoteza mamake  mzazi katika ajali  hiyo
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimtuliza mmoja wa majeruhi baada ya kuondokewa na mama yake mzazi kwenye ajali

Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Bw  Richard  Kasesela  (kulia )  akiwa  na mkuu  wa mkoa  wa Iringa Bi Amina Masenza  wa  kwanza  kushoto na mwenyekiti  wa kamati ya  usalama  barabarani Bw  Salim Asas wakimsaidia mmoja kati  ya majeruhi  wa ajali hiyo Bi Sarafina Mkagasana  Rai wa  Rwanda ambae  alikuwa  mmoja kati ya majeruhi wa ajali  hiyo Bi Sarafia amempoteza  ndugu  yake Janeth Mkashena  katika ajali  hiyo

 Mwenyekiti wa kamati ya  usalama barabarani mkoa  wa Iringa  Bw  Salim Asas  akimjulia hali majeruhi  Sarafina  Mkagasana Raia wa aliyelazwa katika  Hospitali ya Rufaa ya  mkoa  wa Iringa baada  ya kupata ajali ya basi lenye  namba  za  usajili    T 798 AKV mali ya Lupondije Express aliyekuwa amelazwa Hospitalini hapo
Mwenyekiti wa kamati ya   usalama barabarani mkoa  wa Iringa  Bw  Salim Asas kulia akiwa na mkuu  wa wilaya ya  Iringa Bw Richard Kasesela  kushoto  wakisaidia  kupakia  dawa zilizonunuliwa na kamati ya  usalama barabarani kwa ajili ya majeruhi wa ajali  ya basi
 lenye  namba  za  usajili    T 798 AKV mali ya Lupondije Express
 
WANANCHI  wa Manispaa ya  Iringa mkoa  wa Iringa washerekea Pasaka kwa kwa majonzi kufuatia vifo  vya watu  sita   waliokufa   papo  hapo akiwemo aliyekuwa mgombea uenyekiti  wa UVCCM mkoa  wa Iringa Makka Msigwa na  wengine  zaidi ya 20 kujeruhiwa  vibaya  baada  ya  basi lenye  namba  za  usajili    T 798 AKV mali ya Lupondije Express Kutoka  Mwanza kuja  Iringa  kupinduka  eneo la  Mteremko  wa Ipogolo  mjini  Iringa  wakati basi hilo   likielekea  kufaulisha  abiria  wa  Mbeya.



Imeelezwa   kuwa baadhi ya  abiria    waliokufa  katika  ajali   hiyo na  majeruhi   ni  wale ambao   walitakiwa   kushuka stendi kuu ya mabasi  ya mabasi  yaendaye  mikoani mjini Iringa ila dereva  wa basi aligoma   kuwashusha  stendi na  kupitiliza nao  kwenda Ipogolo    kufaulisha abiria  wa Mbeya  kwanza  ndipo arudi   kuwashusha  stendi.



Ajali   hiyo  imetokea  majira ya  saa 3 usiku wa Pasaka  baada ya  basi  hilo  kufeli  breki katika  mteremko  huo huo mkali kabla ya  kupinduka .



Wema  Zuberi  ni  mmoja kati ya majeruhi  wa ajali  hiyo aliyekuwa ametoka mkoani  Dodoma  kuelekea  Mbeya  alimweleza  mwandishi  wa habari hizi    kuwa  mwendo  wa  basi hilo  toka  amepanda  Dodoma  kuja  Iringa  haukuwa  mkali  sana   ulikuwa ni  mwendo wa kawaida .



Japo  alisema  kuwa   baada ya  kuingia  mjini  Iringa katikati ya  mji  ndipo dereva  wa basi   hilo alionyesha  kuendesha basi   hilo kwa mwendo mkali  zaidi  kiasi  cha  baadhi ya  abiria  kulalamika mwendo huo na  kutaka   kushushwa ila dereva  hakuweza  kusikia zaidi ya  kuwapuuza  abiria  hao.



“Abiria  wengi   walionyesha   kumlalamikia   dereva   huyo kwanza  kutokana na  kuwapitiliza  stendi pasipo  kuwashusha na pili mwendo  kasi ambao  alikuwa  akienda nao   ili  kufanikisha  kutufaulisha abiria  tuliokuwa   tukielekea  Mbeya “



Alisema kabla ya  kufika  eneo  hilo ambalo  basi  lilipinduka kuna kona kali na mteremko  mkali  na kilichoonekana haraka  haraka ni  dereva   kushindwa kukata  kona   hiyo baada ya Breki  kufeli   na   hivyo  kulazimika  kuhama  njia  na  kugonga kingo za  barabara  hiyo na  kupinduka .

Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  Bw  Richard Kasesela akizungumza na  mwandishi  wa  habari  hizi eneo la   tukio alisema  kuwa zoezi la  kuendelea  kutafuta  miili  iliyobanwa na basi  hilo imekuwa  ngumu  kutokana na kukosekana  kwa gari la kuinua  basi hilo na  tayari  amemwagiza  meneja  wa Tanesco kuleta  gari  hilo na  iwapo  dereva   hayupo  basi kuamka  na  kuendesha  mwenyewe .



Hata   hivyo  alisema  kuwa kuanzia   sasa  dawa  ya  madereva  hao  ni  kuwashughulikia kwani kama Rai imekwisha   tolewa  mara  nyingi na  bado  ajali  zinaendelea   kutokea.

Kamanda   wa  polisi  wa mkoa  wa Iringa  Bw  Peter Kakamba  ambae  pia  alikuwepo  eneo la  tukio kusaidia  kuokoa majeruhi na kutoa maiti katika basi hilo  pamoja na mkuu  huyo  wa  wilaya wananchi  mbali mbali walioongozwa na askari  polisi ,alisema  kuwa  watu  watano  watu 6  wamepoteza maisha katika ajali  hiyo  huku  majeruhi ni 38 kati yao 11  wameruhusiwa Hospitali

Alisema   kuwa  jeshi la  polisi  linamshikilia  dereva wa basi hilo Kastory Mwalusako (35) mkazi  wa Mbeya ambae baada ya ajali  alijisalimisha  polisi na kuwa atafikishwa mahakamani  wakati  wowote kuanzia  sasa .

Wakati 

Wakati  huo  huo serikali ya  mkoa  wa Iringa  imeipongeza kamati ya  usalama  barabarani mkoa  wa Iringa  chini ya mwenyekiti  wake  Salim Asas kwa  kujitolea msaada wa dawa  za  kuwatibu  majeruhi  wote wa ajali ya basi   hilo.


Mkuu  wa mkoa  wa Iringa  Bi Amina Masenza  alitoa pongezi hizo jana baada ya  kupokea msaada wa dawa  hizo  kutoka kwa  mwenyekiti Bw  Asas kuwa  kamati hiyo  imeonyesha   upendo  mkubwa kwa  majeruhi hao  huku akitaka dawa  hizo kutumika vizuri na  kuhakikisha  zinawanufaisha  majeruhi hao.

Huku kwa upande wake  mwenyekiti wa kamati   hiyo ya usalama barabarani Bw  Asas  mbali ya  kuwapa pole  majeruhi  hao bado  aliwataka  abiria  kutoa ushirikiano kwa  jeshi la  polisi kwa  kutoa taarifa  haraka  pindi  dereva anapo  kuwa anaendesha gari  bila  kuzingatia  sheria  za usalama barabarani na  kuwa iwapo basi hilo  lingeshusha abiria  stendi yawezekana kusingetokea  madhara makubwa  hivyo kwani basi hili lilikuwa  limefika salama Iringa mjini ila dereva  aliendeleza safari ambayo kimsingi haikuwepo .

Jumatano, 23 Machi 2016

MWIGULU NCHEMBA KUHAMISHA UFUGAJI KUTOKA UFUGAJI HOLELA KWENDA UFUGAJI WA VITARU

MWIGULU NCHEMBA KUHAMISHA UFUGAJI KUTOKA UFUGAJI HOLELA KWENDA UFUGAJI WA VITARU

 Picha/Maelezo na Festo Sanga

 

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh:Mwigulu Nchemba akimuangalia mmoja wadume  la ng'ombe anayetumika kuzalisha Mitamba kwenye kitaru namba 9 shamba la kitengule-Karagwe.Baadhi ya ng'ombe waliopo kitaru namba 9 shamba la kitengule ambapo kwenye block hii moja kuna Ng'ombe zaidi ya 800 wanaolishwa na kuhudumiwa vizuri na mmiliki wa kitaru hiki.Ng'ombe wakitoka kuogeshwa kwaajili ya kuua baadhi ya wadudu kama kupe wanaopendelea kukaa kwenye mwili wa ng'ombe.Hili ni moja ya josho la kisasa ndani ya kitaru namba 9.
Kufuatia ziara ya waziri mkuu,Mh:Kassim Majaliwa ndani ya mkoa wa Kagera akiwa ameambatana na waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani,Ziara hiyo imekuja na maagizo kadhaa ikiwamo wamiliki wote wa vitaru kwenye ranchi za Taifa ambao hawajaziendeleza waziachie mara moja na maeneo hayo yagawiwe upya,Waziri Mkuu ameagiza pia kwa wamiliki wa vitaaru ambao sio watanzania wajisalimishe au waondoke kwenye vitaru hivyo kabla hatua kali hazijaanza kuchukuliwa.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh:Mwigulu Nchemba akiwa na timu yake ya wataalamu wameshaanza kupitia vitaru vyote "blocks" na wamiliki wake ikiwepo pia idadinya mifugo kwa kila block,Hii leo Mwigulu Ncheba amekutana na wamiliki wa vitaru kwenye shamba la Kitangile-Karagwe na kuagiza wamiliki wote ambao hawajaendeleza maeneo wanayoyamiliki yanachukuliwa na serikali kwaajili ya kuwapatia watanzania wenye uwezo wa kuziendesha.
Mwigulu Nchemba ameagiza pia wamiliki wa vitaru kuacha mchezo wa kukodisha na kuingiza mifugo kutoka kwa wafugaji haramu wa nchi jirani,kitendo hicho ni kosa na yeyote atakayebainika anakwenda jela na adhabu kali itafuta.
Mbali na vitaru hivyo,Waziri Mkuu akishirikiana na waziri wa kilimo wameagiza ofisi ya mkuu wa mkoa wa kagera kuondoa wavamizi wote kwenye pori tengefu ya serikali kabla hatua zingine zinazofuata kuanza kutekelezwa.
Kupitia uwekezaji mzuri kwenye kitaru namba 9 cha shamba la Kitengule,Mwigulu Nchemba ametoa rai kwa wafugaji wote nchini kuanza kujipanga kufuga kwa mfumo wa vitaru ili kuachana na ufugaji holela unaopelekea migogoro mbalimbali na wakulima.

Taifa Stars vitani leo


Taifa Stars vitani leo


TIMU ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, leo inashuka Uwanja wa Ommisports Idriss Mahamat Ouya jijini ND’jamena kuwavaa wenyeji Chad katika mchezo wa kuwania fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Kikosi cha Stars kikiongozwa na Kocha Mkuu Charles Mkwasa kiliwasili nchini humo kwa ajili ya mchezo huo muhimu kuhakikisha wanapata ushindi wa ugenini kabla ya kurudiana Machi 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Taarifa ya Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto ilimkariri Mkwasa akisema wamejipanga vizuri na wanatarajia kung’ara leo.
“Tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri katika mchezo huu wa ugenini ili tutakaporudi nyumbani tutumie pia vyema uwanja wetu, ” alisema Mkwasa.
Licha ya kukabiliwa na mchezo huo muhimu, kikosi cha Taifa Stars kiliwasili kwa mafungu kutokana na wachezaji wengi kukabiliwa na majukumu katika timu zao, ambapo zilikuwa kwenye michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho mwishoni mwa wiki.
Kwa mujibu wa Kizuguto, kikosi cha Taifa Stars kimekamilika baada ya kuwasili kwa nahodha wa timu hiyo anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta na mshambuliaji Thomas Ulimwengu anayecheza TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Taifa Stars inakutana na Chad ambayo si miongoni mwa nchi zinazojulikana katika soka, ikiwa inashika nafasi ya 127 katika ubora wa viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), huku Tanzania ikiwa ni ya 125.
Hadi sasa Taifa Stars inashika nafasi ya tatu katika kundi hilo la G ikiwa imecheza mechi mbili ikiwa na pointi moja, ambapo ya kwanza ilifungwa mabao 3-0 na Misri mjini Cairo, kisha ikatoka 0-0 na Nigeria Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Misri inaongoza Kundi G ikiwa na pointi sita baada ya kushinda mechi zote mbili ikiifunga Taifa Stars na Chad, wakati Nigeria inashika nafasi ya pili baada ya kuifunga Chad na kutoka sare na Taifa Stars, huku Chad yenyewe ikiburuza mkia baada ya kupoteza mechi zote mbili ilizocheza.
Kwa mazingira hayo ni wazi Taifa Stars ina kila sababu ya kushinda leo na kujiweka katika nafasi nzuri katika michezo ya marudiano kwa kundi hilo.

SHAMBULIO LA BRUSSELS WATU 31 WAPOTEZA MAISHA

SHAMBULIO LA BRUSSELS WATU 31 WAPOTEZA MAISHA


Watu 31 wamefariki baada ya mashambulio kutekelezwa katika uwanja wa ndege wa Zaventem na kituo cha treni cha Maelbeek mjini Brussels.
Waziri wa afya wa Ubelgiji amesema watu 11 walifariki na wengine 81 kujeruhiwa baada ya milipuko miwili kutokea uwanja wa ndege wa Zaventem, nje kidogo ya mji wa Brussels.
Meya wa Brussels amesema watu 20 walifariki Maelbeek.
Kundi linalojiita Islamic State limedai kutekeleza mashambulio hayo
Waziri Mkuu wa Ufaransa Francois Hollande amelaani mashambulio hayo mjini Brussels na kusema ni kama mashambulio yaliyolenga bara lote la Ulaya.
Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel amesema hatua zaidi zimechukuliwa kuimarisha usalama mpakani.Milipuko hiyo imetokea siku nne tu baada ya kukamatwa kwa mshukiwa mkuu wa mashambulio ya Paris ya mwaka jana ambayo yalisababisha vifo vya watu 130.
Abdeslam alikamatwa Ijumaa katika mtaa mmoja wa Brussels.
Uwanja wa ndege wa Zaventem unapatikana kilomita 11 kaskazini mashariki mwa Brussels na ulihudumia abiria zaidi ya 23 milioni mwaka jana.

Musukuma:Tamasha la Pasaka lipige vita mauaji ya vikongwe, albino

Musukuma:Tamasha la Pasaka lipige vita mauaji ya vikongwe, albino


……………………………………….
msukuma
Na Mwandishi Wetu

……………………………………….
MBUNGE  wa Geita vijijini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Joseph Kasheku Musukuma
Amewahi kutamka bungeni kuwa vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi wamekuwa wanauawa wanne kwa wiki kitu ambacho ni kibaya na sio cha kibinaadamu.
Mbunge huyo alisema kuwa kutokana na kampuni ya Msama kutambua umuhimu wake wana kila sababu ya kuwaunga mkono  na angependa kuona wananchi wanajitokeza kwa wingi katika tamasha hilo ili kuzungumza na Mungu kupitia waimbaji na viongozi wa dini katika tamasha hilo litakalofanyika mikoa ya Kanda ya ziwa.
Alisema hiyo ni kama dawa ambayo imekuja kutibu tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe hivyo  anaamini kuwa  nguvu za Tamasha hilo wataweza kusonga mbele.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka Alex Msama alisema tamasha hilo litafanyika mkoani Geita kuanzia Machi 26 kwenye ukumbi wa Desire, Machi 27 kwenye uwanja wa CCM Kirumba na Machi 28 litafanyika uwanja wa Taifa wilayani Kahama.
Waimbaji mbalimbali wamethibitisha kushiriki katika tamasha hilo




UNFPA yakabidhi vifaa tiba vyuo na taasisi za afya nchini.

UNFPA yakabidhi vifaa tiba vyuo na taasisi za afya nchini.

1Mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini Natalia Kanem (aliyesimama) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya kutumia simu kwa ajili ya kufundisha wakunga na wauguzi njia ya uzazi salama, waliokaa kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali) Dkt. Otilia Gowele, Msajili wa Baraza la Uuguzi Lena Mfalila na Geeta Lal kutoka makao makuu ya UNFPA
2Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Dkt. Otilia Gowele akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kuhusu uzazi salama kwa njia ya simu kwa wawakilishi wa Vyuo vya Afya nchini pamoja na Taasisi zinazoshughulikia afya ya mama na mtoto,  waliokaa meza kuu kutoka kulia ni Nayanesh Bhandutia kutoka makao makuu ya UNFPA, Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo ya Wauguzi na Wakunga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Ndementria Vermand, Mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini  Natalia Kanem, Msajili wa Baraza la Uuguzi Lena Mfalila na Geeta Lal kutoka makao makuu ya UNFPA
3Wawakilishi kutoka Vyuo vya Afya na Taasisi zinazojihusisha na uzazi salama nchini  wakifuatilia mafunzo ya uzazi salama kwa kutumia teknolojia mpya ya simu.
4Geeta Lal kutoka Makao Makuu ya UNFPA akitoa maelekezo kwa washiriki (hawapo pichani) kuhusu mafunzo ya uzazi salama ambayo yanapatikana ndani ya simu hiyo.
5Mkuu wa Chuo cha Uuguzi Newala Tecla Ungele (wa kwanza kulia) akipokea seti ya simu ya kufundishia uzazi salama kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Otilia Gowelle , wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini Natalia Kanem

UVCCM WAPONGEZA USHINDI WA DKT.SHEIN

UVCCM WAPONGEZA USHINDI WA DKT.SHEIN.

Na Mwandishi Wetu ,Zanzibar
……………………………………….
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  (UVCCM )umesema ushindi alioupata mgombea wa CCM Rais Dk Ali Mohamed Shein kwamba ni kielelezo cha kuimarika kwa msingi ya demokrasia Zanzibar na kukubalika kwa mgombea huyo kwa wapiga kura na wananchi wa Zanzibar .
Umesema ushindi huo sasa umehitimisha mvutano na maneno yaliyokuwepo ambayo yalikuwa yakienezwa kwa makusudi ,  kupotoshwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani visiwani humu.
10Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka ameeleza hayo Afisi kuu ya UVCCM Kikwajuni wakati akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kumaliza kwa maandano makubwa yaliyoandaliwa na UVCCM kusherehekea ushindi wa CCM uliotangazwa  na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar  Jecha Salim Jecha kulitangaza jina la Dk shein mshindi wa uchaguzi huo.
Alisema ushindi alioupata Dk shein kwa kupata jumla ya kura  299982sawa na asilimia 91.4 kumeidhihirisha dunia jinsi ya kukubalika kwa kiongozi huyo katika aina ya utawala na uongozi wake.
“Ameonyesha umahiri, upeo na uwezo mkubwa  katika kuongoza serikali ya umoja wa kitaifa kwa miaka mitano iliopita; amekuwa mstahamilivu na nguzo muhimu ili jamii isiendelee kugawanyika “alisema shaka
Kaimu Katibu Mkuu alisema aina ya uongozi wa Rais Dk Shein ni wa kipekee na kwamba kama angekuwa si mtawala mwenye maarifa mapana na uvumilivu wa kisiasa serikali hiyo anaamini ingevunjika mapema.
Shaka alisema serikai za mseto za Zimbabwe na Kenya ziliweza kuyumba  na kwamba hazikudumu kutokana na baadhi ya viongozi wake kukosa kuaminiana, kuvumiliana na kustahamiiiana .
11“Ushindi huu ni pigo jipya kwa chama cha CUF ambacho kimesusia uchaguzi wa marudio bila sababu za msingi, ushindi wa Dk shein  naamini utaleta mageuzi makubwa ya kiuchumi  na kuishangaza dunia katika maendeleo ya demokrasia “alisems Shaka
Aidha alisema anatarajia serikali mpya ijayo haitakuwa na viongozi wababaishaji na badala yake watateuliwa wazalendo, wachapa kazi na watu wenye uchungu wa kiyatetea Mapinduzi bila kushiriki usaliti.
Hata hivyo Shaka alisema anaamini kuwa chini ya uongozi wa kipindi cha pili cha utawala Dk Shein na sera makini za ccm ,ataendelea kusimamia uadilifu serikalini,  kujenga umoja wa kitaifa nchini  pamoja na kuwatumikia wananchi ipasavyo na kudumisha huduma za jamii .
13“UVCCM tuna matumaini makubwa na na Dk shein katika awamu mpya ya ushindi wake; ataunda baraza la mawaziri makini, na hatutosita kumpongeza kila atakapofanya vizuri  pia hatutakaa kimya pale tutakapoona mambo  hayaendi ipasavyo “alisema .
Shaka anewahimiza vijana mahali popote walipo kumuunga mkono Dk shein na kuisaidia serikali yake ili iweze kupiga hatua za kimaendeleo na kwamba hatawaangusha katika uongozi wake.
“Tunahitaji kutoka mahali tulipo na kufika tunakotarajia, tungependa kuona uwajibikaji mpya,utendaji wenye kubeba dhamira na utekelezaji wa malengo na sera hivyo ni wazi kuwa   wapatikane watu wenye uwezo na upeo ya kukwamua nchi mahali ilipo sasa”

StarTimes yatoa msaada wa iPad kwa Wizara ya Habari

T1Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Nape Nnauye ( katika) akisalimiana na Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu You Qing wakati alipowasili katika ofisi za Kampuni ya ving’amuzi ya StarTimes kwa ajili ya kupokea msaada wa iPad kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Maafisa Mawasiliano Serikalini, kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang.
T2Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu You Qing (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Nape Nnauye kabla ya sherehe za makabidhiano ya  msaada wa iPad kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Maafisa Mawasiliano Serikalini toka Kampuni ya ving’amuzi ya StarTimes, mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
T3Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiteta jambo na Kaimu Mkurugezi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa wakati wa sherehe za makabidhiano ya  msaada wa iPad kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Maafisa Mawasiliano Serikalini toka Kampuni ya ving’amuzi ya StarTimes, mapema hii leo jijini Dar es Salaam (katikati) ni Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rioba.
T4Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang (katikati) akimtambulisha Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rioba kwa (kushoto) kwa Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu You Qing wakati wa sherehe za makabidhiano ya  msaada wa iPad kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Maafisa Mawasiliano Serikalini toka Kampuni ya ving’amuzi ya StarTimes, mapema hii leo jijini Dar es Salaam

SPIKA NDUGAI AFANYA MABADILIKO YA BAADHI YA WAJUMBE WA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE.


imagesNa Benedict Liwenga-Maelezo.
…………………………………………….
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) amefanya mabadiliko ya baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge ili kuzingatia mahitaji mapya na changamoto zilizojitokeza baada ya kuunda Kamati hizo mwezi Januari 2016.
Taarifa hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Ofisi ya Bunge Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano ambapo imeelezwa kuwa, mabadiliko hayo, yamefanywa chini ya Kanuni ya 116(3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge inayompa Spika Mamlaka ya kuteua Wabunge kuunda Kamati Mbalimbali za Bunge.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, kufuatia mabadiliko hayo ambayo baadhi yake yamehusu Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au wote wawili, Kamati za Kudumu za Bunge zilizoathirika na mabadiliko haya zitawajibika kufanya Uchaguzi wa viongozi kwa mujibu wa kanuni ya 116 (10).
Baadhi ya Kamati ambazo zimeathirika na mabadiliko hayo na ambazo zitawajibika kufanya uchaguzi kwa viongozi ni zikiwemo; Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii ambayo itahitaji kupata Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wapya, Kamati ya Nishati na Madini ambayo itahitaji kupata Mwenyekiti mpya, Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma itahitaji kupata Mwenyekiti mpya, Kamati ya LAAC ambayo pia itahitaji kupata Makamu Mwenyekiti mpya na Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ambayo itahitaji kupata Makamu Mwenyekiti mpya.  
Aidha, taarifa hiyo imeeleza pia mabadiliko hayo kwenye kamati zote yanaanza mara moja ambapo orodha ya wajumbe waliobadilishwa imeshatolewa na Ofisi hiyo na kusambazwa katika vyombo vya habari.

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete awasili Tunis, Tunisia


J1Rais Mstaafu wa awamu ya nne na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika Mgogoro wa Libya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkaribisha Waziri wa Manghreb, nchi za Kiarabu na Afrika wa Aljeria Mheshimiwa Abdelkader Messaleh, aliyemtembelea hotelini kwake katika Jiji la Tunis, Nchini Tunisia.
J2Rais Mstaafu wa awamu ya nne na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika Mgogoro wa Libya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza na Waziri wa Manghreb, nchi za Kiarabu na Afrika wa Aljeria Mheshimiwa Abdelkader Messaleh, aliyemtembelea hotelini kwake katika Jiji la Tunis, Nchini Tunisia.
J3Rais Mstaafu wa awamu ya nne na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika Mgogoro wa Libya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiagana na Waziri wa Manghreb, nchi za Kiarabu na Afrika wa Aljeria Mheshimiwa Abdelkader Messaleh, aliyemtembelea hotelini kwake katika Jiji la Tunis, Nchini Tunisia.
…………………………………………………………………………………….
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika wa Usuluhishi wa Mgogoro wa Libya, amewasili jana Jijini Tunis nchini Tunisia  kushiriki Mkutano wa 8 wa Nchi majirani wa Libya.
Mkutano huo umeitishwa na Serikali ya Tunisia, na ni muendelezo wa jitihada za nchi majirani kusaidia kuleta hali ya amani na usalama nchini Libya.
Rais Mstaafu Kikwete amewasili Tunis akitokea Salalah nchini Oman alikoshiriki Mkutano wa Kamati ya Bunge la Kuandika Katiba ya Libya.
Akiwa Jijini Tunis, Jana tarehe 22 Machi, 2016 Dkt. Kikwete amefanya mazungumzo na Waziri wa Masuala ya Maghreb, nchi za Kiarabu na Afrika, wa Algeria Mheshimiwa Abdelkader Messaleh, aliyemtembelea hotelini kwake.
Katika mazungumzo hayo, Waziri Messaleh amempongeza  Rais Mstaafu Kikwete kwa kuteuliwa na Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika kusuluhisha mgogoro wa Libya. Amemueleza hali ya usalama na kisiasa ya  Libya na mtizamo wa nchi yake juu ya namna bora ya utatuzi wa mgogoro huo, na akamhakikishia ushirikiano wa Serikali ya Algeria katika jukumu lake alilokabidhiwa na Umoja wa Afrika.
Kwa upande wake, Rais Mstaafu Kikwete amemshukuru Waziri Abdelkader Messaleh kwa maelezo yake na ushirikiano aliomuahidi na akamueleza matumaini yake ya kupatikana kwa suluhu ya mgogoro huo hasa ikizingatiwa kuwa nchi jirani na Libya na Umoja wa Afrika zitashirikiana na wadau wote kuhakikisha mgogoro huo unatatuliwa.
Rais Mstaafu Kikwete amesisitiza kuwa suluhisho la kudumu la mgogoro wa Libya liko mikononi mwa wananchi wa Libya wenyewe.
Katika ziara yake nchini Tunisia, mbali na kuhudhuria Mkutano wa 8 wa nchi jirani na Libya,  Rais Mstaafu Kikwete anatarajiwa pia kukutana na Waziri Mkuu Mteule na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Libya,  (Presidency Council) Mheshimiwa Fayez Al-Sarraj,  wadau wengine wa Libya  pamoja na kutembelea Ofisi ya Ujumbe wa Umoja wa Afrika kwa Libya iliyoko jijini Tunis.
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete anatarajiwa kurejea nchini tarehe 25 Machi, 2016.
Imetolewa; Ofisi ya Rais Mstaafu.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Tunis
22 Machi, 2016

JIJI LA DAR ES SALAAM LAPATA MEYA MPYA.

C1Aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Yenga  Yusuph alipokuwa akiomba kura kwa wajumbe walioshiriki zoezi la kupiga kura ya kumchagua Meya leo jijini Dar es salaam.
C7Baadhi ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) walioshiriki zoezi la kupiga kura ya kumchagua Meya wa Jiji leo Dar es Salaam (Kushoto) ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Iddy Azzan Zungu na kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Segerea Mhe. Bonnah Kaluwa.
C6Baadhi ya wapiga kura waliohudhuria uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam Leo 22/03/2016 wakifuatilia uchaguzi huo.
C5Baadhi ya Maafisa kutoka  Ofisi za  Jiji Dar es Salaam wakifuatilia Uchaguzi wa Meya uliyofanyika leo (kwa kwanza kulia) ni  Afisa Sheria Mkuu  Jumanne Mtinangi.
C4Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda Mhe. Agustine Mahiga akizungumza na aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Meya wa Jiji kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Yenga Yusuph.
C3Mbunge wa Viti Maalum  Kinondoni  kupitia  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Suzan Lyimo (kushoto) pamoja na Mbunge wa jimbo la Kawe Mhe. Halima Mdee (CHADEMA) wakifuatilia zoezi la Upigaji kura wa kumchagua  wa Meya leo jijini Dar es Salaam.
C2Mjumbe wana Kamati Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Edward Lowasa akimpongeza mshindi wa nafasi ya Umeya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Chacha mara baada ya kutangazwa mshindi leo jijini Dar es Salaam.
Na Anitha Jonas – MAELEZO
………………………………………………….
Kaimu Mkurugenzi Jiji la Dar es Salaam Bi. Sara Yohana amemtanganza Mhe. Isaya Chacha Diwani wa Kata ya Vijibweni (CHADEMA) kutoka Manispaa ya Temeke kuwa Meya Mpya wa Jiji hilo.
Kaimu Mkurugenzi huyo alimtangaza Isaya kuwa mshindi mara baada ya uchaguzi huo kufanyika leo  jijini Dar es Salaam ambapo mshindi alipata kwa kura 84 dhidi ya mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw.Yenga Yusuph ambaye alipata kura 67 wakati kura 7 ziliharibika katika uchaguzi huo.
“Tunawashuruku wapiga kura wote mlioshiriki zoezi hili la upigaji kura kwa utulivu bila vurugu na kuweza kufanikisha mpaka kumpata Meya wa Jiji hili” alisema Bi Yohana.
Kwa upande wa mshindi wa Kiti cha Meya wa Jiji Mhe. Chacha aliwashukuru wapiga kura wake wa kata ya Vijibweni kwa kumchagua kuwa Diwani pamoja uongozi wa chama chake kukubali kumpa nafasi ya kugombea kiti hicho.
“Nimejipanga kuleta maendeleo katika sekta ya elimu pamoja na kupambana na kero ya foleni katika jiji letu na nitahakikisha wananchi wote maskini wanafaidika  na mapato ya jiji hili ikiwemo kuendeleza miundombinu mbalimbali ,”alisema Chacha.
Aidha, Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Bw.Freeman Mbowe alisema idadi ya wapiga kura tu inaonyesha wazi kuwa ushindi wa kiti hicho cha Meya ni lazima uchukuliwe na  CHADEMA sababu  madiwani wengi wa Mkoa wa Dar es Salaam wanatoka katika chama hicho.

Tigo yatoa msaada wa madawati 500 kwa shule za msingi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda akihutubia wananchi na wanafunzi katika makabadhiano wa msaada
wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za
msingi katika mkoa wa Dar es Salaam

Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda(kulia) na Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez (wa pili kulia),wakiwa wameketi kwenye moja ya madawati 500 yalikabidhiwa na kampuni ya Tigo kwa shule za msingi 10 jijini Dar es Salaam jana. Wengine katika picha  ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani , Goodluck Charles (wa tatu kulia)na Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni, Dkt. Aziz Msuya(kushoto). Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga.

Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez katika makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga.
 Mwanafunzi Saidat Proches akishukuru mara baada ya makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda akiongea na walimu na wananchi mara baada  makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam

Sherehe ya makabidhiano ilifanyika leo shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga

Mgamlagosi wa EWURA AMTEMBELEA SPIKA WA BUNGE


D1Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson akizungumza na Wajumbe wa  Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati Kamati hiyo ilipokutana na  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa.
D2Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson akifuatilia Mjadala kati ya  Wajumbe wa  Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa alipoitembelea kamati hiyo. Anayezungumza  kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Balozi Adadi Rajabu  na (kulia mwenye tai yekundu) ni Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Charles Kitwaga.
D3Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA Bw. Felix Mgamlagosi aliyemtembelea leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
D4Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA Bw. Felix Mgamlagosi aliyemtembelea leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Kulia Ni Afisa Meneja Mahusinao wa EWURA Bw Titus Kaguo.
D5Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsikiliza Meneja Mahusiano wa EWURA Bw Titus Kaguo wakati walipomtemblea Ofisini kwake kati kati ni Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA Bw. Felix Mgamlagosi
(Picha na Ofisi ya Bunge)