Posted by Esta Malibiche on Dec 5,2016 in News
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira pamoja na wachungaji, wakiinua mikono wakati wa ibada ya Kuliombea Taifa Kinziga, Salasala Jijini Dar es Salaam. |
Mwimbaji Alfonsina Samweli wa
kanisa la Assemblies of God la Kinziga Salasala Jijini Dar es Salaam
akimpa Mkono Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Luhaga Mpina, baada ya kumkabidhi kablasha lenye DVDs zenye nyimbo za
Injili wakati wa ibada ya Kuliombea Taifa.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na mazingira Mhe. Luhaga Mpina akikata Utepe katika CD
kuashiria kuzinduliwa kwa Abum ya Nyimbo za Injili za mwimbaji Alfonsina
Samweli.
Sehemu ya waumini wa kanisa la
Assemblies of God la Salasala. Wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina
Hayupo Pichani wakati wa ibada maalumu ya kuiombea Taifa iliyofanyika
Jijini Dar es Salaam. (Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)
………………………………………………………………………
Na Evelyn Mkokoi – Salasala DSM
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina amesema Serikali ya
awamu ya Tano inaongozwa na Nguvu za Mungu katika kuwatumikia wananchi
wake na si vinginevyo.
Pia amesema Serikali ya awamu ya
Tano kamwe haitayumbishwa wala kuyumba katika kutenda yaliyomema kwa
maendeleo ya nchi kwa kuogopa maneno ya watu ya kuwakatisha tamaa.
Akizungumza Dar es Salaam jana
wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la Kusifu na Kuabudu na kuliombea Taifa
la Kanisa la Tanzania Assemblies of God lililopo katika eneo la Kinzugi
Salasala, alisema Serikali itaendelea kusimamia misingi yake bila
kuogopa maneno ya watu wanaoyoikatisha tamaa kwani Sheria na Katiba za
nchi zinatokana na maneno yaliyopo katika vitabu vya Mungu.
Alisema watumishi wa Mungu
wanatakiwa kuwaombea viongozi katika kutenda kazi zao kwani uongozi
waliokuwa nao ni uchaguzi kutoka kwa Mungu na sio kwa nguvu za mtu
yeyote.
” Uongozi unatokana na
Mungu,Mimi Mpina sikujua kama ningekuwa Waziri nilimaliza siku mbili
sikujua kama niliteuliwa kuwa Naibu Waziri kipindi hicho nilikuwa
shambani nikafatwa na kuambia kuwa nimechaguliwa ,nikasema ni uweza wa
Mungu,”alisema na kuongeza kuwa
“Utawala wa awamu ya tano
tunemtanguliza mbele Mungu,tunaomba muendelee kutuombea tutekeleze
majukumu yetu licha ya kuwepo kwa vikwazo mbalimbali katika kutekeleza
majukumu yetu,”alisema Mpina
Aidha aliziomba familia za
wakristo kuwa mfano wa kuigwa katika utunzaji wa mazingira kwani bila
kuwepo kwa mazingira safi magonjwa yatapata nafasi katika jamii.
“Familia za Kikristo lazima ziwe
mfano wa kuigwa katika utunzaji wa mazingira, hizi faini tunazowapiga
watu kutokana na ukiukwaji wa sheria za mazingira kwa uchafuzi wa
Mazingira, sio kama tunawaonea bali kuwakumbusha wajibu wao “alisema
Kwa Upande wake,Mchungaji wa
Kanisa la Assembly of God , Deusi Sabuni alisema watahakikisha
wanaendele kufanya Maombi kuiombea serikali ya awamu ya tano na viongozi
wake.
Alisema roho za uadui zilizopo na
watu kusema vibaya na kuwakatisha tamaa kusiwavunje mioyo kwa
kusikiliza maneno ya watu katika kuleta maendeleo ya nchi kwa manufaa
ya taifahili na watu wake.
“Makanisa na Misikiti tupo pamoja
nanyi katika kuwaombea na kama serikali hii ikiendelea hivi ndani ya
miaka mitatu nchi yetu itabadilika,”alisema Mch.Sabuni.
Ibada maalum ya Kuliombea Taifa,
kusifu pamoja na kuimba, ilienda sambamba na uzinduzi wa Ablum ya nyimbo
za injili za mwimbaji Alfonsina Samweli pamoja na mnadawa kuuza DVDs
zenye nyimbo za injili.
0 maoni:
Chapisha Maoni