Posted by Esta Malibiche on Dec 2,2016 in NEWS
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa
kwa misaada na ushirikiano kwa serikali ya Tanzania ikiwemo huduma kwa
kambi za wakimbizi, Mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana yenye kauli mbiu
ya Vijana - Fursa na misaada mingi katika shughuli za maendeleo Hayo
ameyasema wakati wa mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez aliyemtembelea Mkuu huyo wa mkoa ofisini kwake. RC Makalla
amewahakikishia ushirikiano zaidi kwa mradi wa Vijana kutambua fursa na
kuzitumia utakaotekelezwa Mkoa wa Mbeya mwakani.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (kushoto) akisalimiana na Mratibu Mkazi
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake na kufanya
mazungumzo ya kuboresha ushirikiano baina ya Serikali na Umoja wa
Mataifa jijini Mbeya.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisaini kitabu cha wageni
ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomtembelea ofisini
kwake na kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali
na Umoja wa Mataifa jijini Mbeya.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akielezea dhumuni la safari
yake mkoani Mbeya kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla wakati
alipomtembelea Mkuu huyo wa mkoa na kufanya naye mazungumzo kwa lengo la
kuimarisha ushirikiano baina Umoja wa Mataifa na Serikali.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala akielezea mipango aliyonayo ya kuinua
uchumi wa mkoa wake na kutatua tatizo la ajira kwa vijana ambalo limekua
changamoto kubwa nchini kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez (katikati) aliyemtembelea ofisini kwake akiwa ameambatana na
Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (kushoto).
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa taarifa
zilizomo kwenye Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya
Maendeleo UNDAP II 2016-2021 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla
alipomtembelea ofisini kwake na kufanya naye mazungumzo kwa lengo la
kuimarisha ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na Serikali.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi
rasmi Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya Maendeleo UNDAP
II 2016-2021 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomtembelea ofisini
kwake jijini Mbeya.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na
Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (kulia)
nje ya jengo la ofisi za mkuu huyo wa mkoa.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mkuu wa
mkoa wa Mbeya, Amos Makalla katika picha ya pamoja na "Orange car" ikiwa
ni wiki ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia:
'Elimu kwa wote" nje ya ofisi za mkuu huyo wa mkoa.
Mkuu
wa mkoa wa Mbeya, Amos Makala akiagana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja
wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake na
kufanya naye mazungumzo jijini Mbeya.
0 maoni:
Chapisha Maoni