Posted by Esta Malibiche on Dec 30,2016 in NEWS
Aliyekuwa mtumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (RUNAPA), Emiliyo Mwadila Lugiriva
pichani amemuomba Rais John Pombe Magufuli aingilie kati suala la madai yake ya
kutelekezwa na mwajiri wake, baada ya kustaafu kwa hiari mnamo tarehe
01.07.2007.
Akizungumza na mtandao huu wa Habari mapema leo hii, ametaja baadhi ya madai yake hayo kuwa ni pango la
chumba kimoja ambacho kilihifadhi mizigo iliyoletwa Iringa na kuahidiwa
kusafirishwa hadi sehemu husika yaani, Minjingu, Manyara, pango la vyumba
viwili ambavyo familia ilikua ikishi mjini Iringa kabla ya kupewa nyumba
nyingine kwa ajili ya familia na pango la vyumba viwili ambavyo alitumia baada
kutekelezwa na mwajiri wake tangu tarehe 30.10.2007.
Lugiriva alisema
kuwa mnamo mwezi wa kumi (10) 2007 aliambiwa atasafirishwa hadi nyumbani kwake
(Mijingu), lakini cha ajabu alifikishwa Iringa na kuambiwa hapo ndiyo nyumbani
kwake, wakati nyumbani kwake ni Minjingu wilyani Babati, mkoani Manyara.
Alitaja
madai mengine kuwa ni posho ya kujikimu yeye na familia yake tangu kutekelezwa
na mwajiri huyo pamoja na nauli kutoka Serengeti-Ruaha-Iringa-Tungama lenga-Msembe.
Alisema
kuwa aliomba kustaafu kwa hiari kutokana ya matatizo ya afya yake kwani,
alikuwa anasumbuliwa na magonjwa ya kisukari, vidonda vya tumbo, macho na
masikio.
Lugiriva
alizaliwa mwaka 1952 na mwaka 2007 akiwa na miaka 55, hivyo kutokana na maradhi
hayo yalipelekea utendaji wake kudhoofu ndipo alipoandikia barua ya kustaafu
kwa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadi za Taifa (TANAPA) kuomba kustaafu kwa
hiari.
Aidha,
alisema kuwa aliwahi kuwaandikia barua ya madai Ofisi ya Wizara ya Maliasili na
Utalii tarehe 31.07.2011 bila mafanikio, kwa hivyo amemuomba Rais Magufuli
amsaidie katika suala lake, kwani anateseka na familia yake.
Alisema
kuwa anaomba asafirishwe nyumbani kwako Mijingu wilayani babati, mkoani
Manyara, kwani huko ndio alikozika wazazi wake na baadhi ndugu zake.
Alisema
kuwa katika mazungumzo yake na Kaimu Mhifadhi Mkuu kupitia barua yake tarehe
03.07.2007 kuhusu haki zake, aliambiwa anastahili kupewa ‘Certificate of
Service’ , malipo ya PPF (Pension) pamoja na gharama ya kusafirishwa yeye na
familia yake na mizigo isiyozidi tani 1.5 hadi nyumbani kwake.
Nipashe
ilifanikwa kuongea na mmoja ya viongozi wa Hifadhi ya Taifa Ruaha na kudai
kwamba madai yake (Lugiriva) wanayafahamu na kuongeza kuwa suala hilo
linachanganya.
Kiongozi
huyo alidai kuwa suala la mstaafu huyo linachanganya sana kwa sababu wakati
anaajiriwa alijiandikisha kuwa nyumbani kwake ni Iringa lakini baada ya
kupelekwa Iringa alibadilisha mawazo kuwa kwake ni Minjingi Wilaya ya Babati,
mkoani Manyara.
Alisema
kuwa bwana Lugiriva ametembea sehemu mbalimbali kuhusu suala lake ameenda mpaka
mahakamani lakini bado hajaridhika na majibu yake.
Naye Mkuu
wa Hifadhi ya Taifa Ruaha, Dk. Christopher Timbuka akiongea kwa njia
simu alisema suala hilo kuhusiana mtumishi huyo linaeleweka na kwa sasa
lipo mikono mwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa linashughulikiwa.
Alisema
kuwa masuala waliyamaliza na mkuu wa mkoa na bawana hiyo aliapa kuwa kwao
ni Iringa na sio Mijingu kama anavyodai mtumishi huyo.
Kuhusu
suala la certificate of service nalo alisema kuwa hilo lipo juu hawezi
kulisemea.
0 maoni:
Chapisha Maoni