Jumatatu, 12 Desemba 2016

SHEREHE YAMAULIDI YA KUZALIWA MTUME (M.A.S)

Posted by Esta Malibiche on Dec 12,2016 in NEWS

1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Sheikh Sherali Champsi mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya sherehe ya maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,
2
Baadhi ya Viongozi na waalikwa mbali mbali wakiwa katika Sherehe ya kuadhimisha Maulid ya kuzalia Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,
3
Mke wa Rais wa Zanzibar  Mama Mwanamwema Shein(katikati) akiwa na wake wa Viongozi mbali mbali na Wananchi wakiwa katika sherehe za maadhimisho ya Maulid ya kuzalia Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,
4
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji akimkaribisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) katika  Maulid matukufu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) Sherehe zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,
5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akimuangalia Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji akitia ubani kama ishara ya Kuyafungua Maluid matukufu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) Sherehe zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja.
6
Waislamu na Wananchi waliohudhuria katika sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja,
7
Ustadh Ali Muombwa Hassan wa Chuo cha Kiislamu akitoa Tafsiri ya Qur’aan Tukufu  ya Suratul Touba (Aya 128 hadi 129) iliyosomwa  katika  sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja
8
Wanafunzi wa Madressa Hidayatul Munineema na Nurul Islamia ya Mpendae Mjini Unguja wakisoma Qaswida YaRabii Swali katika sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja,
9
Ustadh Mohamed Khamis Rashid wa Kiweani Pemba akisoma maulid Barzanji mlango wa kwanza katika sherehe tukufu ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja,
[Picha na Ikulu.] 12/12/2016.

0 maoni:

Chapisha Maoni