Jumatatu, 12 Desemba 2016

TBL Mwanza yaunga mkono kampeni ya kupanda miti

Posted by Esta Malibiche on Dec 12,2016 in NEWS

pandaWafanyakazi wa TBL wakipanda miti katika moja ya kampeni ya upandaji miti
………….
 

Kiwanda cha TBL cha Mwanza kimeunga mkono  kampeni ya kupanda miti inayoendelea mkoani Mwanza ambapo kimetoa miche 2,000 ya miti pia wafanyakazi wake wameungana na viongozi wa serikali na wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali kupanda miti katika eneo la Chuo cha Uvuvi .

Meneja Mwandamizi wa TBL,Mwanza,Joseph Malibe, alisema kuwa  kampuni imeunga mkono jitihada  hizi ikiwa ni moja ya utekelezaji malengo ya kampuni ya kulipa suala la mazingira kipaumbele popote inapofanyia biashara zake pia inayo sera ya sera ya wafanyakazi kutumia muda wao kwa ajili ya kazi za kijamii.

Tunafurahi kushiriki katika tukio hili la kupanda miti lililoandaliwa na taasisi ya mazingira ya Tanzania Environmental Conservation Organization (TECO) kwa kuwa linaendana na mtazamo wetu wa kutunza mazingira na vyanzo vya maji”.Alisema   Joseph Malibe.

 

Alisema kuwa TBL itaendelea kuunga mkono jitihada za utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji popote inapoendeshea biashara zake ikiwemo kufanya uzalishaji usio na athari  kwa mazingira.

 

Malibe alisema uzalishaji wa kutumia nishati mbadala tayari unatekelezwa katika viwanda mbalimbali vya TBL “Hapa Mwanza tumeanza kufanya uzalishaji kwa kutumia mitambo inayotumia nishati inayotokana na mashudu ya pamba na pumba za mpunga na katika kiwanda cha Mbeya kimeanza kufanya uzalishaji kwa kutumia umeme wa nishati ya jua”.

 

Alimalizia kwa kutoa wito kwa watanzania wote kujenga utamaduni wa kutunza mazingira ili kupunguza athari kubwa zinazoendelea kujitokeza sehemu mbalimbali duniani kutokana na uharibifu wa mazingira.

 

0 maoni:

Chapisha Maoni