Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza
na watumishi wa Wizara yake wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi
la Wizara katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016. .........................................
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewataka
watendaji na watumishi wa Wizara yake kuzingatia maadili na uwajibikaji
katika utekelezaji wa majukumu yao.
Ameyasema
hayo wakati akifungua Baraza la wafanyakazi la Wizara yake na
kusisitiza kwa watendaji kuwasimamia watumishi walio chini yao
kuzingatia maadili na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao
katika kutoa huduma kwa wananchi.
Ameongeza
kuwa kuwepo kwa ushirikiano kati ya uongozi na watumishi utasaidia
kufanikisha masuala mbalimbali ya maendeleo ya Wizara, Taasisi zake na
watumishi katika kuleta maendeleo ya Wizara katika kutimiza wajibu wao.
“Nawataka
watumishi wazingatie maadili katika kutekeleza wajibu wao na naamini
kwa juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano tutarudisha maadili ya Utumishi
wa Umma na bado taratibu zinaendelea kusimamiwa ipasavyo”asisitiza Mhe
Nnauye.
Mhe.
Nnauye amesisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt John Pombe Magufuli ana mpango wa dhati wa kurujesha maadili katika
Utumishi wa Umma na kuhakikisha heshima yake inarudi.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni