01:52
Posted by Esta Malibiche on Dec 2,2016 in MICHE
Baada ya
wanachama wa klabu ya Yanga kwenda mahakamani kuzuia Mkutano ambao
uliitishwa na Mwenyekiti wao Yussuf Manji kwani walikuwa hawakubaliani
na mchakato mzima wa mabadiliko juu ya kukodishwa timu yao hatimaye Leo
upande wa pili ambao ni kama ni kulwa na Dotto ameibuka na kauli yao
kupitia Baraza la wadhamini la klabu ya Simba SC limeweka kikwazo katika
mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji katika klabu hiyo yenye maskani
yake mtaa wa Msimbazi Dar es Salaam.
Taarifa kwa vyombo vya habari
ambayo imetolewa na mmoja wa wajumbe wa baraza hilo Mzee Hamis Kilomoni
inapinga hoja ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshwaji wa klabu hiyo.
Tazama mambo ambayo yaliyotolewa na na mdhamini huyu kwa kupitia nakala yake:
● Swala la mabadiliko limegawa wanachama na kupandikiza chuki miongoni mwao kufikia hatua ya kupigana na kutozikana.
● wanachama hawakupewa taarifa ya mabadiliko kama agenda ya 9 ya mkutano wa tarehe 31/7/2016 ilivyosema.
Hivyo basi Baraza hilo la wadhamini ambao ndiyo wana mamlaka na mali za Simba SC imeamua kufanya yafuatayo:
1.Kuzuia mkutano wa tarehe 11/12/2016 ulioitishwa na Viongozi wa Simba mpaka uhakiki wa wanachama ufanyike kupitia kwa msajili.
2. Kutolewe elimu ya mfumo pendekezi ya uendeshaji kwa wanachama wote kupitia matawi yao.
3. Kumwomba Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda kusimamisha mkutano huo wa tarehe
11/12/2016 kwani kuna dalili za uvunjifu wa amani.
4. Kuiomba Serikali kuingilia kati mgogoro huu kwa ajili ya usalama wa nchi.
0 maoni:
Chapisha Maoni