Posted by Esta Malibiche on Dec 5,2016 in NEWS
Warsha ya wadau ya usimamizi wa rasilimali za maji na mazingira mjiini ikiendelea Makambako, mkoani Njombe.
Warsha ya wadau ya usimamizi wa rasilimali za maji na mazingira mjiini ikiendelea Makambako, mkoani Njombe.
Warsha ya wadau ya usimamizi wa rasilimali za maji na mazingira mjiini ikiendelea Makambako, mkoani Njombe.
Warsha ya wadau ya usimamizi wa rasilimali za maji na mazingira mjiini ikiendelea Makambako, mkoani Njombe. |
Washiriki wa Warsha wakitoka Nje ya ukumbi mara baada ya kumalizika kwa warsha hiyo,iliyofanyika katika Mji wa Makambako, mkoani Njombe. |
Washiriki wa Warsha wakiwa katika picha ya pamoja |
WANANCHI wameshauriwa kutunza
mazingira hata baada ya wafadhili kumaliza mradi wao kwani kuvunjika kwa koleo
sio mwisho wa uhunzi.
Kauli hiyo imetolewa na maofisa maendeleo jamii wa shirika la kuhifadhi mazingira duniani
(WWF-Tanzania), Martha Sanga na Evergris Makfura wakati wakifunga warsha ya
wadau ya usimamizi wa rasilimali za maji na mazingira mjiini Makambako,
mkoani Njombe.
Walisema katika nyakati tofauti kuwa
wananchi na wadau mbalimbali wa mazingira wanabudi kuendelea hata baada ya
programu ya maji Ruaha kumaliza muda wake, kwani utunzaji wa mazingira ni
jukumu la kila mtu.
Walisema kuwa suala la usimamizi wa
rasilimali za maji na mazingira sio la wafadhili, bali ni jukumu la kila mmoja
kuhakikisha mazingira yanatunzwa.
Shirika la WWF kwa kupitia Programu
yake ya Maji Ruaha (RWP) kwa kushirikiana na Bodi ya Maji Bonde la Rufiji
(RBWB), halmashauri, wananchi na wadau mbalimbali wa mazingira walitekeleza
mradi wa miaka mitano wa katika usimamizi wa rasilimali za maji na mazingira
ambao ulikuwa na lengo la rudisha hali ya Mto Ruaha Mkuu ili uweze kutiririsha
maji kwa mwaka mzima.
Martha na Makfura walisema kuwa bado
mapambano ya utunzaji wa rasilimali za maji na mazingira
yanaendelea hata bila kuwepo wafadhili .
Warsha hiyo ililenga kutathmini
shughuli zilizotekelezwa na wadau mbalimbali wa mazingira kwa kipindi cha miaka
mitano cha utekelezaji ulioratibiwa na shirika la WWF kupitia Programu yake ya
Maji Ruaha kwa kushirikiana na Bodi ya Maji Bonde la Rufiji (RBWB).
Maafisa maenedeleo ya jamii kutoka
Shirika la WWF Tanzania kupitia Programu yake ya Maji Ruaha wamewataka wadau
kuendelea kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji kwa kutumia dhana ya
ushirikishwaji.
Maafisa hao wa jamii walisema kuwa
Serikali ilishaweka sawa mahitaji ya kisheria (legal framework) kama vile
kupitishwa kwa Sheria Mama ya Mazingira (2004), kutolewa kwa Sera ya Maji
(Julai 2002) na Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Namba 11 ya mwaka
2009.
Naye Roy Kadege ambaye pia ni
Mhasibu wa Jumuiya ya Watumiaji Maji (WUA) katika Bonde dogo la Mto Mpando
wilayani Wanging’ombe, mkoani Njombe, alisema kuwa jumuiya hiyo atahakikisha
inasimamia kikamilifu suala zima la usimamizi wa rasilimali za maji na
mazingira.
Alisema kuwa pamoja kuwa mradi
kumaliza muda wake, wataendelea kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa vile
vyanzo vingi vya maji vipo katika ukanda wao na ambako vyanzo vya mito
vinakoanzia.
Alisema kuwa kupitia programu ya
Maji Ruaha, jumuiya hiyo ya watumiaji wa maji imeweza kutoa elimu ya usimamizi
wa rasilimali za maji na mazingira katika vijiji 20 vinavyozunguka bonde dogo
la Mto Mpando.
Alisema kuwa baada ya kuwepo mradi
huo wameweza kutunza vyanzo vya maji na kulikopelekea kurudisha Mto Mbarali
mkoani Mbeya.
Mto huo ulikauka kutokana na
shughuli mbalimbali za kiuchumi zisizo endelevu lakini na kwa uwepo wa mradi
huo wameweza kutunza mazingira.
Naye Adamson Msigala ambaye pia ni
Mwenyekiti wa jumuiya ya watumia maji (WUA) katika bonde la mto Mpando alisema
kuwa ili zoezi la usimamizi wa rasilimali za maji na mazingira ziweze kuwa
endelevu halmashauri hazinabudi kutenga fedha kwenye bajeti zao kwa ajili ya
shughuli za utunzaji mazingira kuliko kutegemea wafadhili.
“Kwa mfano, wadau wetu wa maendeleo
wanamaliza mradi wao haina maana kwamba shughuli za usimamizi wa rasilimali za
maji na mazingira zatasimama rahasha, sasa ni jukumu letu wananchi kwa
shirikiana na halmashauri zetu kuweka mikakati yakuweza kuendelea pale wadau
wetu walipoishia,” alisema Msigala.
Alisema kuwa kigezo cha umaskini
kisiwe chanzo cha kuharibu mazingira ni lazima watu wafanya kazi kutunza
mazingira bila kusukumwa bali kwa moyo.
Aliongeza kuwa wakati WWF wanaleta
mradi huo kwa mara ya kwanza, wananchi walikuwa wagumu kuuelewa kwa vile
walikuwa wamezoea kulima kwenye vinyungu ambavyo ni vyanzo vya maji.
Kwa upande wake, Ofisa Maendeleo ya
Jamii Wilaya ya Wanging’ombe, mkoani Njombe Michael Haule ambaye pia ni timu ya
wawezeshaji ya wilaya (DFT) alilipongeza shirika la WWF kupitia programu ya
maji Ruaha pamoja na Bodi ya Maji Bonde la Rufiji (RBWB) kwa kuwaunganisha
wadau mbalimbali wa mazingira ili kuweza kupanga mipango yao kwa pamoja.
Alipendekeza pia kuwa kwa siku za
usoni kunapokuwa na warsha kama hizo washirikishe na vyombo vya usalama na
mahakama ili waweze kutambua jumuiya za watumia maji kuwa zipo kisheria.
Alisema kuwa bila kushirikisha
vyombo hivyo usimamizi wa rasilimali za maji na mazingira utakuwa mgumu kwa
vile kutakuwa na na mwingiliano wa shughuli baina ya vyombo hivyo na jumuiya za
watumia maji.
Alisema kuwa kuna wakati fulani
jumuiya za watumia maji zilikuwa zikiwakamata waharifu wa uharibifu wa vyanzo
vya maji na wakipelekwa polisi wanatolewa.
Kumbe kungekuwa na ushirikishaji wa
vyombo hivyo na vikatambua kuwa jumuiya za watumia maji zipo kisheria wangeweza
kwenda pamoja.
Aliongeza kuwa Bodi ya Maji Bonde la
Rufiji wanapoitisha mikutano yao wahakikishe wanawaalika taasisi ya kupambana
na rushwa (TAKUKURU), polisi na mahakama ili waweze kuvitambua vyombo hivyo vya
watumia maji ili kusimamia kikamilifu suala zima la rasilimali za maji na
mazingira.
0 maoni:
Chapisha Maoni