Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani alisema Se rikali imeliagiza Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco) kujiandaa kusambaza wataalamu wake katika vijiji visivyo na umeme,
watakaofanya usajili wa wananachi wanaotaka kuunganishwa na nishati hiyo.
''Vijiji 7,873 kati ya vijiji 12,268 Tanzania Bara vinatarajiwa kuunganishwa na nishati ya
umeme kupitia utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya
Tatu unaofanywa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ndani ya miaka mitano.''alisema Mh.Kalemani
|
0 maoni:
Chapisha Maoni