Ijumaa, 30 Desemba 2016

AL-AHLY YANG’ARA,YAWALAZA MAHASIMU WAO ZAMALEK MCHEZO WA LIGI KUU MISRI

Posted by Esta Malibiche on Dec 30,2016 in MICHEZO

al-a
Usiku wa kuamkia leo mji wa Cairo nchini Misri ulisimama dakika 90 kupisha pambano la mahasimu yaani Derby iliyowakutanisha Zamalek ambao walikuwa wenyeji dhidi ya Al-Ahly mchezo wa Ligi Kuu na kushuhudia wageni wageni wakiibuka na ushindi wa magoli 2-0.
Mchezo ulianza kwa ubabe kama zinavyokuaga mechi za watani wengine haikuwachua muda Al-Ahly kupata goli dakika ya 22 kupitia kwa mshambuliaji hatari mwenye uchu wa kufumania nyavu,Moamen Zakaria baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Zamalek.
Licha ya kufungwa goli hilo Zamalek waliendelea kufanya mashambulizi ya kushtukiza ili waweze kusawazisha hata hivyo wageni walikuwa na ulinzi Imara hadi timu zinakwenda mapumziko Al-Ahly walikuwa mbele.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kwa kucheza kwa umakini kupitia maelezo ya makocha wao huku zikifanya mabadiliko ambayo hayakuweza kuwasaidia Zamalek kwani walijikuta wakifungwa goli la pili dakika ya 90 kupitia kwa Junior Ajayi na kusababisha mashabiki wa Al-Ahly wakilipuka kwa shangwe.
Hadi dakika 90 mwamuzi anamaliza Mpira Al-Ahly wameibuka na ushindi wa jumla ya magoli 2-0 na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa kwa mara ya pili.
Kwa matokeo hayo Al-Ahly wamefikisha alama 45 na kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo huku wakiwa wamecheza mechi 17 wakati wapinzani wao Zamalek wapo katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 35 na kucheza mechi 15 wakiwa na viporo viwili na Ligi hiyo itaendelea tena Leo kwa mechi tatu kupigwa.

0 maoni:

Chapisha Maoni