Posted by Esta Malibiche on Dec 30,2016 in NEWS
MGANGA mkogwe wa tiba Ya asili wa
wilayani Njombe mkoani Njombe, Dk Antony Mwandulami akionyesha chanzo cha maji
alichokihifadhi na kukitumia kusambaza maji kwa wananchi wa kijiji chake
cha Itunduma, wilayani humo.
MGANGA mkogwe wa tiba ya asili wa
wilayani Njombe mkoani Njombe, Dk Antony Mwandulami akionyesha kituo cha
kuchotea maji baada ya kuifadhi chanzo cha maji na kuamua
kuyasambaza maji hayo kwa wananchi wa kijiji chake cha Itunduma,
wilayani humo.
Dk Antony Mwandulami ambae ni Mganga mkogwe wa tiba za asili wa wilayani Njombe
mkoani Njombe ametumia zaidi ya Sh
Milioni 65 kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji lilikuwa
likiwakabili wananchi wa kijiji cha Itunduma, wilayani humo.
Akizungumza na Mtandao huu wa Habari ulipomtembelea juzi kijijini na kufanya mahojiano maalum kuhusu namna alivyopambana
na hatimae kufanikiwa kutatua changamoto hiyo ya maji alisema; akiwa
mkazi wa kijiji hicho aliguswa sana na
tatizo la ukosefu wa maji na ndipo alipoamua kukifufua chanzo cha maji hicho
kilichopo mita 200 kutoka brabara kuu ya Njombe Makambako.
Dkt.Mwandulami alisema chanzo hicho
chenye chemichemi nyingi kilikauka kutokana na kukithiri kwa shughuli za
kilimo, ufugaji na ukataji wa miti.
“Nilianza kwa kutumia zaidi ya
Sh Milioni 18 kukirudisha chanzo hicho katika hali yake ya kawaida na kwa
kushirikiana na serikali ya kijiji tukakihifadhi na kukilinda hadi kikaleta
mafanikio yote hayo,” alisema Mwandulami
Alisema baada ya kuanza
kutiririsha maji alilazimika kujenga bwawa pembeni yake, akapandikiza samaki wa
aina mbalimbali na kujenga njia za maji za kisasa kwa ajili ya kilimo cha
umwagiliaji.
“Mbali na bwawa hilo kuwezesha
usambazaji wa maji majumbani na mashambani lakini limetoa ajira inayowaongezea
kipato vijana wanaojishughulisha na uvuvi.Alisema Mwandulami
Aidha alivitaka vijiji vyenye
changamoto ya maji viende kijijini hapo vikajifunze namna bora na rahisi ya
kuhifadhi na kulinda vyanzo vya maji kwa manufaa yao na ya vizazi vijavyo
akisema maji ni uhai na ni maendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji
hicho, Medson Nyagawa alisema kabla ya kushughulikia changamoto hiyo
wananchi wa kijiji hicho walikuwa wanatembea umbari mrefu kutafuta
maji.
Nyagawa alisema kuwa baada ya
tatizo hilo kuwasumbua kwa muda mrefu Dk Mwandulami aliamua kutumia fedha zake
kuhifadhi na kuanza kukilinda chanzo cha maji cha Nyhengeza, alichimba bwawa
katika chanzo hicho, alipeleka umeme na pampu ya kusukuma maji na akajenga
tenki lenye uwezo wa kuhifadhi lita 32,000 za maji.
“Pamoja na kujenga tenki hilo
akatengeneza mtandao wa kusambaza maji kwa wananchi na kwa ajili ya kilimo cha
umwagiliaji,” alisema huku akimshukuru mganga huyo kwa mchango huo kwa jamii
inayomzunguka’’.Alisema Nyagawa
Mmoja wa vijana anayefanya
shughuli ya uvuzi katika bwawa hilo, Samsoni Mwinami alimshukuru Dk Mwandulami
akisema mchango wake huo, umemuhakikishia kupata wastani wa Sh 10,000 kila siku
kutoka katika shughuli yake yake ya uvuvi katika bwawa hilo.
0 maoni:
Chapisha Maoni