Jumatatu, 19 Desemba 2016

Tanzania ya Viwanda; NSSF, PPF waanza kutekeleza ujenzi wa kiwanda cha sukari.

Posted by Esta Malibiche on 19,2016 in Teknolojia

 pp4

pp1
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama (kushoto) na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (katikati) wakijadili masuala pamoja na wakurugenzi wakuu wa mifuko hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF,  Profesa Godius Kahyarara na Bw.William Erio pamoja na Mbunge Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Omari Mgumba (kulia) kuhusiana na mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari kitakachojengwa katika eneo la Mkulazi, mkoani Morogoro ikiwa ni  uwekezaji wa pamoja  wa mifuko hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF wakati viongozi hao walipotembelea mradi huo mwishoni mwa wiki. 
pp2
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango wakikagua ujenzi wa barabara   inayoelekea sehemu ya mradi ambayo inafanyiwa ukarabati mkubwa na kampuni ya ujenzi ya SUMA JKT.
pp3
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama (wa tatu kushoto) na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (katikati) wakifuatilia maelezo kutoka kwa muwakilishi wa kampuni ya Mkulazi Holding inayotekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari kitakachojengwa katika eneo la Mkulazi, mkoani Morogoro ikiwa ni  uwezeshaji wa pamoja  wa mifuko hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF wakati viongozi hao walipotembelea mradi huo mwishoni mwa wiki. 
  pp5
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama (kushoto) na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (katikati) wakimsikiliza Mbunge Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Omari Mgumba (kulia) ambae jimboni kwake ndipo unatekelezwa  mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda hicho.
  pp7
Wananchi wa kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakikaribisha ugeni huo muhimu. Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 100,000 huku kipaumbele kikiwekwa zaidi kwa wakazi wanaoishi maeneo jirani na mradi.
pp8
Wananchi wa kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakikaribisha ugeni huo muhimu. Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 100,000 huku kipaumbele kikiwekwa zaidi kwa wakazi wanaoishi maeneo jirani na mradi.
pp9
Wananchi wa kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakikaribisha ugeni huo muhimu. Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 100,000 huku kipaumbele kikiwekwa zaidi kwa wakazi wanaoishi maeneo jirani na mradi.
pp10
Washirika muhimu! Wakurugenzi wakuu wa mifuko hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF,  Profesa Godius Kahyarara (kulia) na Bw.William Erio (kushoto) wakisikiliza hotuba ya  Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini mwishoni mwa wiki.
pp11
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakati alipotembelea mradi huo mwishoni mwa wiki ambapo aliwahakikishia wakazo hao kuhusiana na utekelezaji wa mradi huo huku akiwaahidi kuwa mradi utatoa kipaumbele zaidi kwa wakazi wa eneo hilo hususani vijana.
pp12
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama (wa pili kulia) na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (wa tatu kulia) walipotembelea bwawa la Kidunda lililopo kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini. Mawaziri hao walipokea ombi la kuwezesha ujenzi wa daraja litakalounganisha kijiji hicho na Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani ili kurahisisha mawasiliano baina ya mikoa hiyo miwili.
pp13
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama (kushoto) na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (kulia) wakijipongeza baada ya kukamilisha ziara hiyo muhimu. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko hifadhi ya jamii wa NSSF Profesa Godius Kahyarara.
pp14
Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa mfuko hifadhi ya jamii wa PPF  Bw.William Erio
 pp6
……………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu, 
MIFUKO ya hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF imeanza utekelezaji wa awali wa mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari kitakachojengwa katika eneo la Mkulazi, mkoani Morogoro ikiwa ni jitahada ya mifuko hiyo kwa pamoja kuunga mkono muelekeo wa serikali ya awamu ya tano wa kuwekeza kwenye uchumi wa viwanda.
Kukamilika kwa kiwanda hicho kinachotajwa kuwa kitakuwa ni kikubwa zaidi Afrika Mashariki, kutaongeza uzalishaji wa sukari wa hapa nchini ambapo zaidi ya tani laki mbili (200,000) zitakuwa zikizalishwa kwa mwaka sambamba na kutoa ajira zaidi ya 100,000 kwa hatua ya awali.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakati alipotembelea mradi huo mwishoni mwa wiki, Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama aliekuwa ameambatana na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango, mbali na kuipongeza mifuko hiyo, aliwahakikishia wakazo hao kuhusiana na utekelezaji wa mradi huo huku akiwaahidi kuwa mradi utatoa kipaumbele zaidi kwa wakazi wa eneo hilo hususani vijana.
“Mradi huu una ushawishi mkubwa kutoka kwa Rais John Magufuli kutokana na adhma yake ya kuibadili Tanzania kuwa nchi ya viwanda na umekuja kwa wakati muafaka. Nataka huu uwe wa mfano,’’ alisema Waziri Mhagama ambae pia aliambatana na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Stephen Kebwe, Mbunge Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Omari Mgumba pamoja na wawakilishi wa kampuni ya Mkulazi Holding inayosimamia utekelezaji wa mradi huo pamoja na viongozi wengine wa serikali.
Waziri Mhagama aliwaomba watekelezaji wa mradi huo kuainisha  mapema aina ya rasilimali watu watakaohitajika kwenye mradi ili waanze kuandaliwa mapema kuepuka suala la kuagiza wataalamu kutoka nje ya nchi kuja kufanya kazi ambazo zingeweza kufanywa na wataalamu wa ndani iwapo wangeandaliwa mapema.
Kwa upande wake Waziri Mpango alisema tayari serikali imeshatenga sh bilioni 17 katika mwaka wa fedha 2016/2017 kwa ajili ya kumalizia fidia na mipaka kwa wakazi wanaoishi kwenye shamba la miwa kwa ajili ya kiwanda hicho lenye ukubwa wa ekari 63,000.
“Lengo kubwa hapa ni kuzalisha sukari itakayotuwezesha kukidhi mahitaji yetu ya ndani na kuuza nje ya nchi pamoja na bidhaa ambatano ikiwemo ethanol. Pia nitoe wito kwa vijana wa eneo hili kuhakikisha wanakuwa katika vikundi ambavyo vitawawezesha kutekeleza kwa urahisi miradi mbalimbali ikiwemo kuanzisha mashamba yatakayosaidia kuongeza malighafi kwa kiwanda hiki,’’ alisema.
Zaidi Dk. Mpango aliwataka viongozi wa serikali wilayani humo wakiwemo wahandisi  kuhakikisha wanatoka maofisini ili kukagua ujenzi wa miundombinu inayoambatana na mradi huo ikiwemo barabara inayojengwa na kampuni ya ujenzi ya SUMA JKT kuelekea eneo la mradi.
“Ile barabara ndio itatumika kusafirisha bidhaa mbalimbali kutoka na kuelekea kiwandani na iwapo itatengenezwa chini ya kiwango kutokana na uzembe tu wa kushindwa kumsimamia mkandarasi hatutaelewana,’’ alisema Dk Mpango huku akiionya kampuni ya SUMA JKT kutekeleza mradi huo kwa viwango vya ubora ili kulinda imani ya serikali kwa makampuni ya umma katika  utekelezaji wa miradi yake mbalimbali.
Kwa upande wake Dr Kebwe mbali na kuahidi kuusimamia vema mradi huo hadi kukamilika kwake, alitoa wito kwa vijana wa eneo hilo kuhakikisha  wanafanya kazi badala ya kuwategemea zaidi wakina mama na wazee kwenye shughuli za uzalishaji.
“Ninazo takwimu zinazoonyesha kuwa katika kata hii wakina mama na wazee ndio wanaofanya kazi zaidi kuliko vijana na kwa mujibu wa takwimu hizo wakina mama na wazee wanafanya kazi kwa asilimia 68 huku vijana mpo…mbadilike!,’’ alionya.

0 maoni:

Chapisha Maoni