Mchezaji Francis Godwi mzee wa matukiodaima aliyeipatia ushindi timu
ya waandishi wa habari kwa kufunga goli la kichwa na kufanya kuibuka
na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya CDTI
.............................................................
Na MatukiodaimaBlog
TIMU
ya soka ya wanahabari mkoani Iringa IMFC) imezidi kutoa kichapo
kwa timu inazokutana nazo baada ya jana kuidhibu vikali timu ya chuo
cha maendeleo ya jamii (CDTI) Ipogolo Iringa kwa jumla ya magoli 3-2
hivyo kujiweka sawa kwa mchezo wake wa kirafiki kati ya washindi wa
kombe la Spanest 2016 utakaopigwa jumapili kwenye uwanja wa hifadhi ya
Taifa Ruaha .
Humu mashindano ya Mdegela Cup
yakirugugika baada ya pepo kujiinua katikati ya mchezo kati ya usharika
wa kanisa kuu ya Mkimbizi kwa wachezaji kuacha kucheza mpira na kuanza
kuchapana ngumi .
Katika
mchezo huo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa chuo cha CDTI
Ipogolo mchezo uliokuwa kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake na
mabingwa wa mashindano ya Spanest Cup 2016 timu ya KItisi Fc ,
wanahabari waliweza kuonyesha soka lenye upinzani mkali kwa
wanachuo hao kiasi cha wachezaji wa timu ya chuo kuonyesha jazba kwa
kucheza rafu dhidi ya wanahabari hao .
katika
mchezo huo hadi dakika ya 80 kipindi cha pili timu zote zilikuwa
sare ya goli 2-2 kabla ya wanahabari kufanya mabadiliko kwa
kumuingiza mchezaji Francis Godwin ambae ni mwandishi wa gazeti hili
mkoani Iringa na kufanikiwa kufunga goli la ushindi dakika ya 85
kipindi hicho cha pili goli lililofungwa kwa ufundi mkubwa kwa
kichwa na kuwaacha mashabiki na wachezaji wa timu ya chuo midomo
wazi.
Hadi
mwamuzi wa mchezo huo anapuliza filimbi ya mwisho dakika ya 90 timu
ya wanahabari iliweza kutoka uwanjani hapo ikiwa na furaha kubwa
baada ya wanachuo kushindwa kusawazisha goli hilo la lalasalama .
Akizungumza
mara baada ya mchezo huo Fredy Mgunda mwenyekiti wakamati ya ufundi
wa timu ya wanahabari pamoja na kupongeza jitihada binafsi
zilizoambatana na ufundi mwingi toka kwa mchezaji Godwin bado alisema
timu hiyo toka imeanza mechi zake za kirafiki kati ya mechi zaidi ya
tano iliyopata kucheza ni mchezo mmoja pekee ndio walifungwa goli
moja bila ila yote imekuwa ikiongoza .
Hivyo
alisema matumaini ya timu hiyo kuendelea kufanya vizuri zaidi na
jumapili ijayo wamejipanga kuipokonya ubingwa timu ya Kitisi Fc
ambao ni mabingwa wa mashindano ya kupinga ujangili ya Spanest Cup ambao
watakutana na timu hiyo ya wanahabari Iringa .
Alisema
kwa ujumla timu yake imekamilika na ipo vizuri uwanjani na kuwa
sanjari na kuwa na wachezaji wengi wenye vitambi ila bado wachezaji
hao ndio ambao wanafanya vizuri uwanjani na wanafukuza mpira kuliko
wachezaji wa timu pinzani ambao hawana vitambi .
Wakati
huo huo mashindano ya Mdegella Cup yameingia doa baada ya mchezo kati
ya timu ya usharika wa kanisa kuu na Mkimbizi kuvunjika kutokana na
mratibu wa mashindano kushindwa kuzingatia kanuni za soka kwa yeye
mwenyewe kujipa uratibu ,mwamuzi na mchezaji wa timu ya Dira ambayo
inashiriki mashindano hayo.
Mchezo
huo ulioanza kwa lawama nyingi katika uwanja wa Gangilonga jana
kipindi cha kwanza kilimalizika vizuri pasipo vurugu zozote ila
kipindi cha pili hali ya utulivu ilianza kuonekana baada ya usharika
wa kanisa kuu kufungwa goli moja ambalo hakuna aliyepiga ila bado mmoja
kati ya wachezaji wa Mkimbizi alimfuata mchezaji wa kanisa kuu na
kumpiga kichwa na mchezaji mwingine alipokwenda kuamua aliishia
kichapo hali iliyopelekea uwanja huo kugeua ulingo wa ngumi kama dakika
5 hivi kabla ya mwamuzi huyo ambae kuvunja mchezo huo .
Mratibu
wa mashindano hayo Petro Mponzi kuonyesha uvunjaji wa wazi wa
kanuni za soka la mashindano hayo pasipo kushirikisha kamati ya
mashindano juu ya mchezo huo kuvunjia aliiita timu ya Mkimbizi kati
kati ya uwanja na kuipa ponti tatu jambo ambalo limeonyesha wazi
mashindano hayo kukosa usimamizi mzuri kutokana na mtu mmoja kuongoza
nafasi zaidi ya tatu kama uamuzi , uratibu , uchezaji na hata kamati
ya maamuzi hutoa mwenyewe .
Hadi
sasa timu ya usharika wa kanisa kuu ipo njiapanda kuendelea na
mashindano hayo na inataraji kukutana wakati wowote ili kuangalia
kama inaendelea na mashindano hayo ama kujiondoa na sababu kubwa na
uratibu mbovu wa mashindano hayo ambao ulilalamikiwa toka kabla ya
kuanza kwa mashindano hasa namna ya wachezaji wanavyopatikana hali
mratibu huyo akidai mtu yeyote anaweza kucheza bora awe msharika wa
sharika husika jambo ambalo lilipelekea Mkimbizi kuchukua wachezaji
wasio na maadili ya Kikristo na hivyo kuvuruga mchezo huo
|
0 maoni:
Chapisha Maoni