HaLMASHAURI
ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa imefanikiwa kutekeleza Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini kuanzia zoezi la utambuzi, uandikishaji, uhakiki
na malipo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Hayo yamesemwa na Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Kilolo, Grace
Killo
wakati akizungumza na mtandao huu wa Habari [Blog ya KALI YA HABARI] katika mahojiano
maalum kuhusu kaya masikini
zinavyonufaika na TASAF
Killo alisema kuwa jumla ya kaya maskini 6,464 zilitambuliwa na kujengewa uwezo katika vijiji 70 vilivyo kwenye mpango.
'''Ugawaji wa ruzuku katika vijiji 70 vilivyo kwenye mpango
umesababisha kuongezeka kwa mzunguko wa fedha kwenye vijiji hivyo na
kusababisha kukua kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi'''''alisema killo.
Alisema
kuwa baadhi ya kaya nufaika zimefanikiwa kuanzisha miradi midogo midogo
kwa ajili ya kukuza kipato ili waweze kujitegemea hata baada ya mradi
kuisha kwa mfano; ufugaji wa kuku, mbuzi na shughuli za kilimo cha
mbogamboga.
“…Uhamasishaji
umefanyika ili walengwa wajiunge na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) hadi
kufikia Novemba jumla ya Kaya 3,878 kati ya kaya 6,401 zilijiunga na
mfuko wa afya ya jamii sawa na asilimia 60.6, uhamasishaji unaenedelea,”
alisema Killo.
Alisema
kuwa kaya maskini zilizotambuliwa na kuwezeshwa kupata huduma za afya,
malezi, chakula na elimu mpaka sasa kiasi cha fedha zilizotolewa ni
shilingi 1,602,245,272.72.
'''Zipo changamoto zilizojitokeza
katika utekelezaji wa mpango kama vile baadhi ya Kaya kutotumia fedha
kulingana na malengo ya mpango wa TASAF, kwa mfano; kutojiunga na CHF na
kutoanzisha miradi midogo midogo kwa ajili ya kuongeza kipato''alisema Killo
Hata hivyo alisema kuwa baadhi ya kaya zilishindwa kusimamia mahudhurio ya shule na
kliniki kwa watoto kwa asimilia 80 kama muongozo wa TASAF unavyoelekeza.
Alisema kuwa changamoto nyingine ni pamoja na miundo mbinu mibovu ya barabara na mawasiliano ya simu kwa baadhi ya vijiji.
Aidha aliongeza kuwa halmashauri hiyo inapokea kiasi cha fedha kisichotosheleza
kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji wa mpango kwa ngazi ya wilaya na
vijiji ukilinganisha na hali halisi ya mahitaji.
''''Ili
kuweza kutatua changamoto hizo halmashauri inaendelea kuzijengea uwezo
Kaya nufaika juu ya utumiaji wa fedha kulingana na malengo ya mpango kwa
kutumia kamati za Usimamizi za Jamii (CMCs), wawezashaji ngazi ya
Wilaya (PAA Facilitators), uongozi wa kijiji kwa ujumla pamoja na
kusisitiza kupeleka watoto shule na kliniki''alisema '''Kaya 92kati ya 6,464
zimefariki kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kuzolota kiafya na
kuwa na umri mkubwa kwa baadhi ya kaya'''alisema killo
|
0 maoni:
Chapisha Maoni