Posted by Esta Malibiche on Dec 22,2016 in NEWS
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkabidhi
Hati ya Kumiliki Ardhi Bibi Ester Lukondo mkazi wa Bunda Mkoani Mara,
ambaye ni miongoni mwa wakazi 154 waliopelekewa Hati hizo na Waziri wa
Ardhi Wilayani Bunda badala ya wakazi hao kuzifuata Mkoani Mwanza.
Wananchi
wa Musoma mjini wakikwasilisha Kero zao za migogoro ya ardhi kwa Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ili aweze
kuzipatia ufumbuzi.
Wananchi
wa Bunda wakikwasilisha Kero zao za migogoro ya ardhi kwa Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ili aweze
kuzipatia ufumbuzi.
Waziri
Lukuvi akikagua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Buhare wilayani Musoma lenye jumla ya
nyumba 50 zinazokaribia kukamilika.
Waziri
Lukuvi akikagua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Buhare wilayani Musoma lenye jumla ya
nyumba 50 zinazokaribia kukamilika.
Jengo
la Biashara la Musoma Mjini lililojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) ambalo Waziri Lukuvi alifika kuangalia maendeleo yake.
Jengo
la Biashara la Musoma Mjini lililojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) ambalo Waziri Lukuvi alifika kuangalia maendeleo yake.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwa ndani ya jengo hilo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwa ndani ya jengo hilo.
Na. Hassan Mabuye (Kitengo cha Mawasiliano - Wizara ya Ardhi)
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkabidhi
Hati 154 za Kumiliki Ardhi kwa wakazi wa wilaya ya Bunda Mkoani Mara
wakati alipofanya ziara ya siku mbili ya utatuzi wa Migogoro ya Ardhi
mkoani humo.
Lukuvi
alitoa hati hizo kwa wananchi wa Wilaya ya Bunda ili kuwarahisishia
wakazi hao utaratibu wa kupata hati zao pale walipo badala ya kuzifuata
Mkoani Mwanza katika ofisi za Kamishana Msaidizi wa Ardhi Kanda ya
Ziwawa.
Aidha,
Katika ziara hiyo Waziri Lukuvi ametatua migogoro ya Ardhi ya wananchi
wa Musoma mjini na wananchi wa Bunda walio na kero za migogoro ya ardhi
na kuzipatia ufumbuzi pamoja na kupokea vielelezo vya kero za wananchi
zaidi 300 walizoziwasilisha kwa Waziri ili azitolee maamuzi.
Waziri
Lukuvi alikagua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Buhare wilayani Musoma lenye jumla ya
nyumba 50 zinazokaribia kukamilika, ambapo alimtaka Meneja wa Mradi wa
NHC mkoa wa Mara Frank Mambo kukamilisha mradi huo ndani ya miezi
mitatu.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anaendelea
na Ziara zake za utatuzi wa Migogoro ya Ardhi nchini, ambayo imejikita
zaidi katika kutatua migogoro ya ardhi ya Mikoa ya kanda ya Magharibi,
Kaskazini na ile ya Kanda ya Ziwa hapa nchini.
Aidha,
Mhe. Lukuvi baada ya ziara hiyo anatarajiwa kuwasili mkoani Arusha
ambapo pia atatua migogoro ya ardhi inayoukabili mkoa huo katika wilaya
za Arumeru na Karatu.
Hadi
sasa Mhe. Lukuvi ndani ya mwezi huu wa Desesmba ameishatatua migogoro ya
ardhi ya Mkoa wa Kigoma na wilaya zake za Kigoma mjini, Kasulu na
Kibondo na katika Mkoa wa Shinyanga na wilaya zake za Kishapu na
Shinyanga mjini na katika mkoa wa Geita amefanya ziara katika wilayani
Chato
0 maoni:
Chapisha Maoni