Posted by Esta Malibiche on Dec 12,2016 in NEWS
Manispaa
ya Kigoma Ujiji imeazimia kuwashirikisha wananchi wake katika mipango
ya maendeleo na kubadli utamaduni uliokuwepo wa kuitegemea Serikali
kuwaletea mipango yake.
Hayo yamesemwa Jijini Paris na Mratibu
wa Mpango wa Uendeshaji wa Serikali kwa Uwazi (OGP) Kigoma, Mhandisi
Sultan Ndaliwo wakati wa kufunga Mkutano wa Kilele wa mpango huo OGP.
Mhandisi Ndaliwo amesema ushirikishwaji
huo utasaidia kutatua changamoto zinazojitokeza kwa wananchi bila
kuwepo kwa ukiritimba kwani masuala hayo yatakuwa yanajulikana wazi kwa
wananchi.
“Nimefurahishwa na jinsi jiji la
Paris linavyowashirikisha wananchi wake katika kupata maendeleo yao
jambo ambalo tutaenda kulitumia Kigoma,” alisema Ndaliwo.
Ameongeza kuwa anaamini Kigoma Ujiji
inakwenda kubadilika kutokana na utekelezaji wa Mpango Mkakati
waliojiwekea unatekelzwa ipasavyo.
Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya
Ujiji Kigoma, Sultani Hussein Luhavi amesema ataenda kuweka mfumo wa
utoaji taarifa kwa haraka ambapo kunatokea tatizo katika eneo lolote
ndani ya Manispaa ili lifanyiwe kazi na wahusika (tracking system).
Amezishauri Manispaa nyingine zijenge
utamaduni wa kuwasilkiliza wananchi na kuwashirikisha ipasavyo katika
mipango ya maendeleo.
“Utendaji wa jinsi hii utabadilisha Manispaa yetu na kuifanya ipige hatua kubwa katika maendeleo,” alisema Luhavi.
Luhavi amezitaka Manispaa na Halmashauri za Miji nchini kuiga mfano wa Manispaa ya Ujiji Kigoma ili kuharakisha maendeleo yao.
Halmashauri ya Manispaa ya Ujiji Kigoma ni Kati ya Manispaa 15 duniani zilizojiunga na OGP kama manispaa na si nchi.
Manispaa nyingine zilizojiunga na
Mpango huo ni pamoja na Austin ya Marekani; Bojonegoro, Indonesia;
Buenos Aires, Argentina; Elgeyo Marakwet, Kenya; Jalisco, Mexico; La
Libertad, Peru; Madrid, Spain; Ontario, Canada; Paris, France; Sao
Paulo, Brazili; Scotland, Uingereza; Sekondi-Takoradi, Ghana; Seoul,
Korea Kusini and Tbilisi, Georgia.
0 maoni:
Chapisha Maoni