Posted by Esta Malibiche on Dec 12,2016 in NEWS
Waziri
wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Lameck Nchemba amewataka Watanzania wote
nchini kuungana kwa pamoja na kuwataja watu ambao wamekuwa wakifanya
vitendo vya vurugu kwa kuhusisha vitendo hivyo na dini kwani watu hao
wanaweza kusababisha nchi kupoteza amani.
Waziri Nchemba ameyasema hayo katika
sherehe za kitaifa za Maulid ambazo zimefanyika mkoani Singida ambapo
alisema mtu ambaye anamcha Mungu hawezi kuwa akijihusisha na vitendo
hivyo na Serikali ya awamu ya tano itakuwa ikimchukulia hatua mhusika
bila kuhusisha dini.
“Wizara yangu inahusika na taasisi zote
zinazohusika na ibada, niwambie jambo moja tutofautishe udini na kumcha
Mungu, mtu anaposhika sana dini ni mshika dini na mtu unanayemcha Mungu
ni mchaMungu sio mdini, makosa yote katika nchi yanafanywa na makundi
mawili ya watu wenye dini na wasio na dini,
“Kosa lolote ambalo likifanywa liwe
kosa la ambae alifanya kosa, sio kosa la dini, akifanya Mkristo kosa la
mtu sio la dini, akifanya Mwislamu kosa ni lake si la dini, na hata kama
hana dini kosa ni lake yeye, na tusaidiane kuwa tunawafichua
wanaosababisha vurugu,” alisema Nchemba.
Pia Nchemba ametumia nafasi hiyo
kueleza kuwa amekabidhi msaada wa mabati 1,000 kwa ajili ya kutumika
kujenga misikiti na kuahidi kuwa baada ya wiki moja atawapatia gari aina
ya Noah.
0 maoni:
Chapisha Maoni