MBUNGE wa viti maalum
mkoa wa Iringa Suzan Mgonukulima
(Chadema) amempongeza Rais Dkt John Magufuli
kwa kuwapigania
wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama
machinga nchini kwa kutaka
wasinyanyasike kuwa ndicho
kilikuwa kilio cha chama
cha Demokrasia na maendeleo (chadema) katika kuona machinga hawanyanyasiki ila ashauri
wawekewe maeneo yao .
Akizungumza leo alisema kuwa,
siku zote machinga
wamekuwa ni watu wa kunyanyasika katika nchi yao
hali iliyopelekea Chadema wakati wa Kampeni za uchaguzi mwaka 2010 kutumia majukwaa yake ya kampeni kueleza ni namna gani ambavyo chama hicho
kingewapigania machinga .
Mgonukulima alisema
uamuzi wa Rais Dkt Magufuli wa
kuruhusu machinga kufanya kazi
popote bila kufukuzwa na mtu ni uamuzi mzuri ambao
umejibu kilio cha Chadema na machinga hao ambao walikuwa
wakinyanyasika zaidi.
''Pamoja na machinga kutakiwa
kufanya kazi popote ila
ilipendeza serikali kutenga eneo maalum kwa ajili ya machinga hao
ili kuwawezesha wafanyabiashara ambao wamekodi ofisi kwa ajili ya kufanya biashara nao kuweza
kufanya biashara maana shida
iliyopo ni wafanyabiashara wakubwa ambao ndio
wanaolipa kodi mamlaka ya mapato
Tanzania (TRA) kuyumba kiuchumi iwapo machinga watafanyabiashara nje ya maduka
yao''alisema Mgonukulima
Aidha aliongeza kuwa inawezakana
kukawa na muda ama siku maalum
kwa machinga kufanyabiashara katika maeneo yaliyotengwa ili kuwawezesha wafanyabiashara wakubwa nao kufanya biashara na kama itabaki
hivi hivi upo
uwezekano wa wafanyabiashara wakubwa
kujiingiza katika biashara ya umachinga kama njia ya kukwepa kulipa kodi.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni