Posted by Esta Malibiche on Dec 30,2016 in SIASA
Na Rhoda Ezekiel- Kigoma,
KAMATI
ya usalama na maadili na kamati ya siasa ya Wilaya ya Kasulu imetoa
adhabu kwa Mbunge wa Viti maalumu wa Mkoa wa kigoma,Josephin Ngezabuke
na madiwani sita wa Halmashauri ya mji wa Kasulu kwa tuhuma za kuchochea
mgogoro wa madiwani kumpinga Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu
kwamba aondolewe hafai.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari jana katibu muenezi wa Wilaya ya Kasulu Masoud
Kitowe alisema kumekuwa na mgogoro Mkubwa uliodumu kwa miezi mitano wa
Baadhi ya madiwani wa Act na CCM waliomuandikia barua Mkurugenzi ya
kudai Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Kasulu aondolewe hafai na
Chama Cha mapinduzi hakikupatiwa barua hiyo ambayo ingeweza kuwasaidia
kujua chanzo cha tatizo nini.
Alisema
katika mgogoro huo madiwani wa CCM walio shiriki ni watano na kati ya
hao mmoja ambaye ni Seleman diwani wa kata ya Kumnyika amepewa adhabu ya
kalipio ambayo ataitumikia kwa miezi 18 kwa kosa na kushiriki kuandika
barua ya kumkataa mwenyekiti wa Halmashauri hiyo wakati jambo hilo bado
halijajadiliwa katika Kikao cha Chama kwamujibu sisi kama chama tulipo
pata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi tuliwaita madiwani walio husika na
kupewa onyo.
Aidha
kitowe alisema madiwani wanne waliojiorodhesha kwenye barua ya kushiriki
kumpinga Mwenyekiti huyo kamati ya siasa pia imetoa adhabu ambayo kwa
Mujibu wa Sheria za Chama cha mapinduzi hairuhusiwi kuitangaza hazarani
nao watatumikia adhabu hiyo kwa miezi 12.
Alisema
Madiwani hao walipo hojiwa walikili mgogoro huo una chochewa na baadhi
ya watu ambao ni Diwani wa Kata ya Murusi Steward Zinduse ambae alikuwa
akigombea nafasi ya Mwenyekiyi wa halmashauri akashindwa pamoja na
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Kigoma Josephini Ngezabuke nao pia
wamepewa adhabu ambayo hairuhusiwi kutangazwa kwa mujibu wa sheria na
barua walishapewa zinazo elezea adhabu zao.
Hata
hivyo Kitowe alitaja sababu zinazo pelekea Mbunge huyo kumkataa
Mwenyekiti wa halmashuri ni kwamba aliwahi kumuomba meya wa kasulu
ashiriki vikao vya halmashauri ya Mji wa Kasulu baada ya kukataliwa
kwakuwa ni mjumbe wa Baraza la madiwani kakonko alijenga chuki na
Mwenyekiti huyo ,jambo la pili alimuomba mea amuite Everina diwani wa
viti maalumu kwa madai avuliwe madaraka ya udiwani viti maalumu kutokana
na migogoro ya kifamilia kati yake na diwani huyo wa viti maalum.
"Kwa
mbunge wetu huyu migogoro ni kawaida yake ukiona kasulu kuna migogoro
ujue kuna watu wanaochochea, ikumbukweMwaka 2010 kamati ya Siasa ya Mkoa
ilimpa azabu ya kalipio mbunge huyo kutokana na migogoro kwakuwa yeye
anadai anawatu juu watatengua adhabu hiyo ndio maana anaendelea na
migogoro hiyo inayo pelekea Halmashauri kushindwa kufanya Shughuri za
maendeleo suala ambalo hatulifurahii sisi kama Chama.
Alisema
Madiwana hao watano baada ya kupewa adhabu waliachana na mgogoro huo
lakini mpaka sasa Mbunge huyo pamoja na Diwani wa Kata ya Murusi alie
kosa nafasi hiyo bado wanaendeleza Mgogoro huo suala ambalo halina
masilahi katika chama zaidi ya kudhohofisha halmashauri yetu ya Mji wa
Kasulu.
Kwa
upande wake Mbunge wa Viti maalumu Josephin Ngeza buke alisema hawezi
kwenda kwenye halmashauri ya kasulu kuingia kwenye kikao na kufanya
vurugu kwakuwa sheria ninazifahamu ninauwezwa kufanya vurugu hata nikiwa
nje siwezi kupiga kura sehemu mbili yeye ni Mjumbe wa Halmashauri ya
kakonko anacho hitaji ni yeye kupewa heshima kama Mbunge wa Mkoa anapo
fika katika Halmashauri ya Wilaya ya kasulu nikeshimike kama Mbunge.
" mimi
sio kwamba simuhitaji Mweenyekiti sina shida na mwenyekiti wala kurudi
kwenye Baraza la mji wa kasulu mimi nitabaki Kakonko lakini ninacho
hitaji niheshima mimi kama mwenyekiti wa UWT na Mbunge wa Mkoa
mzima,Siwezi kuleta malalamiko yangu kwamba mtu kanifanyia vurugu
nyumbani kwangu nisisikilizwe na hata Zinduse mwenyewe amekwisha ridhika
na Mwenyekiti",alisema Ngezabuke.
0 maoni:
Chapisha Maoni